Foreign Exchange Rates

Ascon Africa advert_6th Dec. 2018

Stanbic Bank - Uhuru Banking - 5th Nov. 2018

CMTL Advert - 5th Nov. 2018

Thursday, 30 June 2016

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA 40 YA KIMATAIFA YA SABASABA


Banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likiwa katika maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara, yanayofanyika kila mwaka katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam tayari limeanza rasmi kutoa huduma zake katika viwanja hivyo.
Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bi Edith Nguruwe akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la (NHC) kuhusina na huduma zinazotolewa na Shirika hilo.
Afisa Mauzo mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Emmanuel Lyimo (kushoto), akimuelezea mwananchi kuhusiana na mradi wa SAFARI CITY uliopo Arusha alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba.
Afisa Biashara wa NHC, Clara Lumbanga, akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wananchi aliotembelea banda hilo kuhusiana na uzwaji wa nyumba. Katikati ni Afisa Mauzo wa NHC, Joseph Haule.
Afisa Mauzo wa NHC, Jasson Ipyana akimuelezea mwananchi kuhusina na miradi ya nyumba ya bei nafuu ilioko nchini.
Afisa Mauzo wa NHC, Wilson Sanane (kushoto), akifafanua miradi mbalimbali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Afisa Mauzo, Aika Swai (kushoto), akielezea kuhusiana na utaratibu wa unaoutumika katika ununuzi wa nyumba za (NHC) huku baadhi ya wadau kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakimsikiliza kwa umakini.

Full Shangwe Blog

No comments:

Post a Comment