Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 9 February 2016

BENKI YA NMB YAWAFIKIA WAKAZI WA TURIANI, YAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI MTIBWA

Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 60 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa shule ya Msingi Mtibwa iliyo katika kata ya Turiani – Mvomelo mkoani Morogoro. Huu ni mwendelezo wa benki kujali wateja na jamii inayozunguka matawi yake huku ikiamini kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wake wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni waliojiwekea.

Kwa mwaka huu – 2016 NMB imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kusaidia jamii katika Nyanja za elimu na afya pamoja na kusaidia vipaumbele vilivyowekwa na serikali kwenye elimu ikiwa ni pamoja na Tehama na maabara kwa shule za msingi na sekondari.

Meneja wa Tawi la NMB Turiani akikabidhi madawati kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mtibwa - Enock Kagonji huku Mwanafunzi wa darasa la sita Nasma Seif akishuhudia tukio hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtibwa wakiwa wamekalia madawati waliyopewa na NMB.
Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki – Nazaret Lebbi akikata utepe kuashiria kuanza kwa matumizi ya madawati yaliyokabidhiwa na NMB kwa shule ya msingi mtibwa.







No comments:

Post a Comment