Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 17 October 2015

MWONEKANO WA SASA WA NYUMBA ZA NHC MWONGOZO BEACH HOUSING ESTATE

Picha za nyumba za miradi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ya Mwongozo zilizopo Kigamboni jijini Dar es Salaam zilizopo katika hatua za mwisho kukamilika.

Baadhi ya nyumba za mradi wa Shirika la Nyumba la Taifa Mwongozo Beach Housing Estate ambao ni mradi wenye nyumba 216, zinavyoonekana kwa sasa.
Hizi ni nyumba za ghorofa za Mwongozo Beach Housing Estate ambao ni mradi wenye nyumba 216, zinavyoonekana kwa sasa.








Mradi wa Shirika la Nyumba la Taifa Mwongozo Beach Housing Estate ni mradi wenye nyumba 216 ikichanganya nyumba za chini za pande mbili na zile za ghorofa moja za pande mbili, nne na sita, upo kilomita 19.5 kutoka kivuko cha Kigamboni, eneo la Mradi likiwa limepakana kwa karibu kabisa na bahari ya Hindi. Takriban nyumba zote zimeshauzwa kwa wananchi.

Mwongozo Housing Estate imejengwa na kujitosheleza kwa huduma zake za msingi kama zahanati, shule ya chekechea na maduka kwa ajili ya wakazi wake. Mradi wa Mwongozo Housing Estate unatarajiwa kuchukua wakazi zaidi ya 1,000 kupitia nyumba 216 zinazouzwa.

Nyumba za Mwongozo Housing Estate zimetenganishwa sehemu mbili za familia tofauti, moja ikiwa na vyumba viwili vya kulala na nyingine ikiwa na vyumba vitatu vya kulala, jiko la kisasa, sebule kubwa na mahali pa kulia chakula. Pia kila nyumba inajitegemea na ina eneo kubwa la maegesho ya magari. Nyumba zinajengwa kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa ili kumuwezesha mnunuzi kufurahia maisha ndani ya nyumba ya kisasa.

No comments:

Post a Comment