Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 29 September 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA MKUTANO WA 70 WA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK, MAREKANI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa 70 wa Umoja wa Mataifa akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushurikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe Sophia Simba, Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Yussuf Mzee na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula.
Rais Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Lars Loekke Rasmussen.
Rais Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Finland Mama Tarja Halonen.
Rais Kikwete na ujumbe wa Tanzania Waziri wa Mambo ya Nje na Ushurikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe Sophia Simba, Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Yussuf Mzee, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.
Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Bahamas Mhe Perry Christie. Hapo Mhe Rais alimfahamisha Waziri Mkuu huyo kwamba yeye anamaliza muda wake na Waziri Mkuu akaeleza matumaini yake kwamba atakayemrithi ataendelea kuimarisha uhusisno wa Tanzania na Bahamas na nchi za Caribbean.
Rais Kikwete akiwa na Rais Filipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji na mawaziri wao wa nchi za nje.
Rais Kikwete na Ujumbe wake wakimlaki Baba Mtakatifu Francis alipowasili kuhutubia Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza. Picha kwa hisani ya Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment