Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 24 March 2015

MTEJA WA BENKI YA NBC TAWI LA BUKOBA, AKABIDHIWA ZAWADI KUBWA YA GARI LA PROMOSHENI YA 'WEKA UPEWE'

Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Pius Tibazarwa (katikati) akikabidhi funguo kwa mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe, Josephat Ruyongo mkazi wa Bukoba, ya gari lake jipya alilojishindia la Nissan Hardbody katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NBC, Musa Jallow. Gari hilo lina thamani ya zaidi ya sh milioni 54.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Musa Jallow (kulia) akimpongeza mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe, Josephat Ruyongo, mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari lake jipya aina ya Nissan Hardbody jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa benki hiyo, Pius Tibazarwa. Gari hilo lina thamani ya zaidi ya sh milioni 54.
Mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya Benki ya NBC, mkazi wa Bukoba, Josephat Ruyongo akifungua gari lake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa NBC, Pius Tibazarwa (katikati), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NBC, Musa Jallow.
Mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya Benki ya NBC, mkazi wa Bukoba, Josephat Ruyongo akiwasha gari lake tayari kwa safari ya Bukoba mara baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam leo.
Mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya Benki ya NBC, mkazi wa Bukoba, Josephat Ruyongo (katikati) akipozi kwa picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo mara baada ya kukabidhiwa gari lake.

No comments:

Post a Comment