Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 20 January 2015

UONGOZI WA ARSENAL WAZURU KWA KUENDELEZA SOKA NCHINI

Afisa Mtendani Mkuu wa Kampuni ya EAG Group, Iman Kajura (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akiutambulisha Uongozi wa Timu ya Soka ya Arsenal kutoka nchini Uingereza, uliokuja Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha na kuendeleza soka hapa nchini. Mkutnao huo ulifanyika kwenye hoteli ya Southan Sun jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Maendeleo wa Timu ya Soka ya Arsenal, Sam Stone na katikati ni Meneja Mahusiano na Maendeleo wa timu hiyo, Daniel Willey.

Uongozi wa Timu ya Soka ya Arsenal kutoka nchini Uingereza umezuru Tanzania kwa ajili kuhamasisha na kuendeleza soka hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Mkurugenzi wa Uhusiano na Maendeleo wa timu hiyo, Sam Stone amesema kuwa Tanzania ni nchi ya sita kwa ukubwa katika bara la Afrika hivyo watasaidia katika kukuza soka nchini.

Amesema leo watakuwa na mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malizi juu ya uendeleza soka nchini.

Amesema katika ziara hiyo wanatarajia kukutana na makampuni 20 kwa ajili ya masuala ya biashara katika kuongeza uwigo zaidi kati timu na wadau wengine katika nchi ya Tanzania.

Kwa upande wa Meneja wa Uhusiano na Maendeleo wa timu ya Arsenal Daniel Willey, amesema wataendelea kutafuta wadau zaidi na kuendeleza soka nchini kwani Tanzania ni nchi ambayo ni kubwa na inaweza kwenda mbele katika mafanikio ya soka.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment