Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Friday, 18 July 2014

BENKI YA KCB YAJIKITA ZAIDI KUSAIDIA JAMII

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa, Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick(katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa misaada ya vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa benki ya KCB Tanzania mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro. Wakisikiliza kwa makini ni meneja wa tawi la Moshi benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo(kushoto), Kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo(wapili kulia), ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo na katibu tawala msaidizi, afya na ustawi wa jamii, Dkt. Mtumwa Mwako. 

Meneja wa tawi la Moshi benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo(kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi misaada ya vifaa vya hospitali yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi-Moshi mjini. Kushoto kwake ni Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa, Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick, Kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo na katibu tawala msaidizi, afya na ustawi wa jamii, Dkt. Mtumwa Mwako.

Kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo(kulia) akitoa shukurani zake kwa niaba ya mkoa baada ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa benki ya KCB Tanzania kwa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi mjini Moshi. Pamoja naye ni meneja wa tawi la Moshi benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo(kushoto) na mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick.


Meneja wa tawi la Moshi, benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo(wapili kushoto) akishikana mikono na kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo(kushoto) kama ishara ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 15 katika hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi mjini Moshi. Wakifurahia tukio hilo ni mganga mfawidhi hospitali ya Mawenzi, Dkt. Lwezaula Fredrick(kulia) na katibu tawala msaidizi, afya na ustawi wa jamii, Dkt. Mtumwa Mwako.

Mteknolojia mionzi, Gerald Shuware(kushoto) akimuonesha kaimu katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Alfred Shayo (kulia) namna mashine ya 'Ultra Sound' inavyofanya kazi baada ya benki ya KCB Tanzania kukabidhi msaada huo na vifaa vingine vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi mjini Moshi. Katikati ni meneja tawi la Moshi, benki ya KCB Tanzania, Oforo Erasmo. 

Mkazi wa kata ya Rau, Michael Mauki akizungumza na waandishi wa habari juu ya changamoto walizokuwa wakizikabili kabla ya kuwa na mashine ya Ultra Sound katika hospitali ya Mawenzi mjini Moshi. Mauki alisema wakazi wa Moshi mjini walilazimika kwenda hospitali za mbali kwa ajili ya kufuata kipimo hicho cha Ultra Sound.

Baadhi ya madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi, wafanyakazi wa KCB Tanzania mjini moshi na wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro, moshi mjini wakifatilia kwa makini hafla ya kukabidhiwa kwa misaada ya vifaa vya hospitali kutoka kwa benki ya KCB Tanzania kwa hospitali ya rufaa ya mkoa, Mawenzi Moshi mjini.

No comments:

Post a Comment