Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Thursday, 2 July 2026

VODACOM YAIMARISHA MCHANGO KATIKA UKUAJI WA UCHUMI KUELEKEA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Dar es Salaam – Vodacom Tanzania Plc, kampuni pekee ya mawasiliano iliyoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), imetambuliwa kuwa mmoja wa walipa kodi wakubwa nchini, hatua inayoakisi dhamira yake ya kuendesha biashara kwa uwazi, uwajibikaji na kwa kuzingatia sheria huku ikiendelea kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Tuzo hiyo, iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inatambua mchango mkubwa wa Vodacom Tanzania katika ulipaji wa kodi pamoja na nafasi yake muhimu katika kuchochea maendeleo ya taifa kupitia uwekezaji na ubunifu.

Akipokea tuzo ya Mlipakodi Bora katika Sekta ya Mawasiliano wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Walipa Kodi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire alisema mafanikio ya kampuni hayaishii katika kutoa huduma bora za mawasiliano pekee, bali pia yanajidhihirisha kupitia mchango wake katika maendeleo ya taifa.

Alieleza kuwa Vodacom imeendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia ulipaji wa kodi, uwekezaji katika miundombinu ya kidijitali, kuendeleza ubunifu, pamoja na kukuza rasilimali watu ili kuimarisha uchumi wa kidijitali.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, utambuzi huo unaimarisha dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuharakisha mageuzi ya kidijitali yanayowanufaisha Watanzania wote.

Wakati Tanzania ikiendelea kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Vodacom Tanzania imeahidi kuendelea kuwekeza katika teknolojia za kidijitali, miundombinu ya mawasiliano na maendeleo ya ujuzi wa kidijitali ili kuharakisha ujumuishi wa kidijitali, kuongeza tija na kuchochea ukuaji wa uchumi shirikishi.

Kwa zaidi ya miaka 20, Vodacom Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuendesha mageuzi ya kidijitali nchini kwa kuunganisha mamilioni ya Watanzania, biashara na taasisi kupitia huduma za mawasiliano na suluhisho bunifu za kidijitali. Kupitia uwekezaji wake endelevu, kampuni imechangia kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kifedha na kidijitali, hivyo kuwa mshirika muhimu katika safari ya maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Utambuzi huu kutoka TRA unathibitisha nafasi ya Vodacom Tanzania kama si tu kampuni inayoongoza katika sekta ya mawasiliano, bali pia mshirika wa maendeleo anayechangia ujenzi wa uchumi jumuishi, shindani na unaotegemea teknolojia kuelekea kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

No comments:

Post a Comment