| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitazama huduma mbalimbali zilizokuwepo ndani ya banda la Vodacom, wakati wa kutembelea banda hilo muda mfupi kabla ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA), baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Philip Besiimire, kuhusu huduma zinazotolewa na kampuni hiyo. Rais Samia aliambatana na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Daniel Chapo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo. Katika hafla hiyo, Vodacom Tanzania ilitunukiwa tuzo mbili ikiwemo Tuzo ya Nafasi ya Tatu katika Kundi la Washindi wa Jumla wa Maonesho hayo na Tuzo ya Nafasi ya Pili ya Udhamini, ikiwa ni kutambua mchango mkubwa kama mshirika muhimu wa Maonesho hayo. Tukio hilo lilifanyika Julai 3, 2026, katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment