Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Thursday, 2 July 2026

NMB YASOGEZA HUDUMA KAMILI ZA KIBENKI KWA WANANCHI KATIKA SABA SABA 2026

Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, William Nkuna (katikati, mwenye shati jeupe), akimwelekeza Afande Bwakiswa Mwakeja kuhusu huduma zinazopatikana katika Tawi la NMB Saba Saba katika kipindi chote cha maonesho. Kushoto ni Jumanne Magige Richard, Afisa Mauzo wa Benki ya NMB.

Dar es Salaam – Benki ya NMB imezindua rasmi huduma za Tawi la NMB Saba Saba, likiwa kituo kamili cha huduma za kibenki ndani ya Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi, wafanyabiashara na waoneshaji katika kipindi chote cha maonesho.

Tawi hilo, lililopo katika makutano ya Mitaa ya Mabalozi na Carnivore, Kitalu Na. 24C, litatoa huduma kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026, likihudumia maelfu ya wageni wanaotembelea maonesho hayo ya kila mwaka.

Huduma zinazopatikana katika tawi hilo ni pamoja na kufungua akaunti mpya, kuweka na kutoa fedha, kufanya malipo mbalimbali ya Serikali, huduma za bima, ushauri wa mikopo pamoja na huduma za kidijitali zinazorahisisha miamala ya kifedha.

Mbali na huduma za kibenki, NMB pia inaendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kuweka akiba, ukopaji wenye uwajibikaji pamoja na usalama wa miamala ya kidijitali. Aidha, tawi hilo lina mashine ya ATM yenye uwezo wa kuweka na kutoa fedha, huku mawakala wa NMB wakisambazwa katika maeneo mbalimbali ya viwanja vya maonesho ili kuongeza urahisi wa upatikanaji wa huduma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hizo, Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, William Nkuna, alisema hatua hiyo inawezesha wananchi, wafanyabiashara na waoneshaji kupata huduma zote muhimu za kibenki bila kulazimika kutoka nje ya Viwanja vya Saba Saba.

"Tawi la NMB Saba Saba linafanya kazi kama tawi kamili katika kipindi chote cha maonesho. Tumefungua rasmi huduma zake kwa umma ili wananchi, wafanyabiashara na waoneshaji wapate huduma za kibenki, elimu ya fedha na ushauri wa kitaalamu," alisema Nkuna.

Aliongeza kuwa wataalamu kutoka vitengo mbalimbali vya benki wanapatikana kutoa ushauri kuhusu mikopo ya biashara, kilimo na ujenzi, huduma za bima, ufunguzi wa akaunti pamoja na matumizi ya huduma za kidijitali za NMB Mkononi Super AppNMB Tap to Pay na NMB UmeBIMA.

Kwa mujibu wa Nkuna, wateja wanaokidhi vigezo wanaweza kupata mikopo ya kidijitali ya hadi Shilingi milioni 2, huku wafanyabiashara wanaostahili wakiwezeshwa kupata hadi Shilingi milioni 5 kupitia simu zao za mkononi bila dhamana na bila kulazimika kutembelea tawi jingine la benki.

Alibainisha kuwa NMB imekuwa mshiriki wa kudumu wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo, na mwaka huu imeongeza thamani ya ushiriki wake kwa kuanzisha tawi linalotoa huduma kamili za kibenki kwa kipindi chote cha maonesho.

Hatua hiyo inaakisi dhamira ya benki ya kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi, kukuza ujumuishi wa kifedha na kuhamasisha matumizi salama ya huduma rasmi za fedha, huku ikitoa suluhisho la haraka kwa mahitaji ya kifedha ya wafanyabiashara na wageni wanaohudhuria Maonesho ya Saba Saba 2026.


No comments:

Post a Comment