Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Tuesday, 30 June 2026

RAIS SAMIA AITUNUKU NMB KWA MCHANGO MKUBWA WA GAWIO SERIKALINI

- NMB yatwaa tuzo baada ya kuikabidhi Serikali gawio la Sh96.9 bilioni -

Dar es Salaam, Juni 30, 2026 – Benki ya NMB imetunukiwa Tuzo ya Mchangiaji Bora wa Gawio baada ya kuikabidhi Serikali gawio la Sh96.9 bilioni, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika kuongeza mapato ya Taifa na kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Tuzo hiyo ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla rasmi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Jumanne, Juni 30, 2026, iliyowakutanisha viongozi wa taasisi na mashirika ya umma pamoja na yale ambayo Serikali ina umiliki wa hisa.

Benki ya NMB iliwakilishwa katika hafla hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, CPA David Carol Nchimbi, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna, waliopokea tuzo hiyo kwa niaba ya benki.

Utambuzi huo unaonyesha nafasi muhimu ambayo NMB inaendelea kuwa nayo katika kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia gawio, kodi na michango mingine ya kisheria inayoiwezesha Serikali kugharamia huduma za kijamii na miradi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa katika hafla hiyo, hadi Juni 29, 2026, Serikali ilikuwa imekusanya jumla ya Sh1.32 trilioni kutoka taasisi na mashirika mbalimbali. Kati ya fedha hizo, Sh800 bilioni, sawa na asilimia 60 ya makusanyo yote, zilitokana na gawio kutoka taasisi zilizopata faida.

Makusanyo hayo yameongezeka kwa Sh300 bilioni, sawa na ongezeko la asilimia 30, ikilinganishwa na Sh1.02 trilionizilizokusanywa kufikia Juni mwaka jana.

Tuzo hiyo inaendelea kuimarisha hadhi ya NMB kama moja ya taasisi zinazoongoza nchini kwa kubadili mafanikio ya biashara kuwa manufaa ya moja kwa moja kwa Serikali, wanahisa na wananchi kupitia mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Kwa miaka kadhaa sasa, NMB imeendelea kuwa miongoni mwa walipa kodi wakubwa nchini na mmoja wa wachangiaji wakuu wa gawio kwa Serikali, jambo linaloakisi utendaji wake mzuri wa kifedha pamoja na dhamira yake ya kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa.



No comments:

Post a Comment