Dar es Salaam, Aprili 23, 2026 — Kampuni ya SanlamAllianz Life Insurance (Tanzania) Limited imezindua rasmi bidhaa mpya ya kifedha iitwayo Salama Plan, ikiwa ni suluhisho mahsusi kwa Watanzania wanaokaribia au waliokwisha kustaafu, ili kuwapatia kipato cha uhakika maisha yao yote pamoja na usalama wa kifedha wa muda mrefu.
Uzinduzi huo ulifanyika katika hafla maalum jijini Dar es Salaam, ukilenga kujibu hitaji linaloongezeka miongoni mwa wastaafu la kuwa na chanzo cha mapato endelevu na kinachotabirika.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtendaji Mkuu wa SanlamAllianz Tanzania, Julius Magabe, alisema:
“Uzeeni unapaswa kuwa muda wa kupumzika, si wa kuwa na wasiwasi. Kupitia ‘Salama Plan’, tunawawezesha watu kufurahia matunda ya kazi zao kwa kujiamini, bila hofu ya kutokuwa na uhakika wa fedha.”
Jinsi Salama Plan Inavyofanya Kazi
Salama Plan ni mpango wa kifedha unaomruhusu mteja kuweka fedha kwa mkupuo (one-time premium) na kisha kuanza kupokea malipo ya mara kwa mara kulingana na mpangilio atakaouchagua.
Kiasi cha chini cha kujiunga ni Shilingi milioni 5, bila ukomo wa kiwango cha juu, jambo linaloifanya bidhaa hii kufikika kwa wigo mpana wa wateja — hasa wale wanaojiandaa kustaafu au waliokwisha kustaafu.
Ulinzi kwa Mteja na Familia
Mbali na kutoa kipato cha maisha kwa mstaafu, mpango huu pia unalenga kulinda ustawi wa familia. Endapo mteja atafariki, wanufaika walioteuliwa wataendelea kupokea malipo kwa kipindi kilichobainishwa.
Aidha, Salama Plan inajumuisha kipengele cha dhamana (guarantee period) kinachohakikisha kuwa mapato yanaendelea kulipwa hata baada ya kifo cha mteja ndani ya muda huo wa dhamana.
Walengwa wa Mpango
Bidhaa hii imelenga zaidi watu wenye umri kati ya miaka 50 hadi 70, wakiwemo:
- Wastaafu kutoka sekta ya umma na binafsi
- Wajasiriamali wanaopunguza shughuli zao za kiuchumi
- Watu wasiokuwa na mifumo rasmi ya pensheni lakini wenye akiba au mali
Akisisitiza umuhimu wa mpango huo, Magabe aliongeza:
“Tunaelewa changamoto zinazowakabili wastaafu wengi, ikiwemo jukumu la kusaidia familia pana na kupanda kwa gharama za maisha. ‘Salama Plan’ ni namna yetu ya kuwaambia mmefanya wajibu wenu, sasa ni wakati wa kufurahia hatua inayofuata ya maisha.”
Hatua Mpya kwa Maandalizi ya Ustaafu
Uzinduzi wa Salama Plan unaashiria mwelekeo mpya kwa Watanzania katika kupanga maisha baada ya ajira, kwa kutoa suluhisho linalochanganya kipato cha uhakika na ulinzi wa kifamilia. Hafla hiyo pia ilijumuisha mijadala ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa pensheni, viongozi wa jamii na washauri wa kifedha, ikiimarisha nafasi ya SanlamAllianz kama mshirika anayeaminika katika mipango ya kustaafu nchini.
Kuhusu SanlamAllianz Tanzania
SanlamAllianz Tanzania ni miongoni mwa kampuni zinazoongoza nchini katika utoaji wa huduma za bima ya maisha, bima za mali na uwekezaji. Kampuni hii inaundwa na taasisi tatu kuu:
- SanlamAllianz Life
- SanlamAllianz General
- SanlamAllianz Investments
Kwa pamoja, zina uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika kuhudumia soko la Tanzania, zikitoa suluhisho za kifedha zinazolenga kulinda maisha, mali na uwekezaji kwa watu binafsi, biashara na taasisi mbalimbali.
Mawasiliano:
Davis Mwijage
Mkuu wa Masoko na Mahusiano – SanlamAllianz Life Insurance
Simu: +255 756 866 010
Barua pepe: davism@sanlamallianz.co.tz

.jpeg)

No comments:
Post a Comment