Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Saudi Arabia (Sadi Fund for Development-SFD), kwa mchango wake katuika maendeleo ya Tanzania kupitia ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za maji, afya, nishati na ujenzi wa miundombinu ya barabasra.
Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo alipo kutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Fund, Bw. Sultan Al-Mashard, Kando ya Mkutano wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji, lililofanyika Mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.
Dkt. Nchemba aliyeambatana na Mawaziri wenzake wawili katika kikao hicho, akiwemo Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, alisema kuwa ushirikiano wa Saudi Arabia na Tanzania uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 sasa, umekuwa wa mfano.
Aliitaja baadhi ya miradi iliyoleta mageuzi makubwa katika jamii ya Tanzania kuwa ni pamoja na ukarabati wa Mradi wa Maji mkoani Mara (Usd 15m), Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe (Usd 25m), na ujenzi wa Barabara za Vijijini Awamu ya Pili-Zanzibar (Usd 11.4m).
Aliitaja miradi mingine kuwa ni Ukarabati na Upanuzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar (Usd 15m) na kushirikiana na wadau wengine kufadhili Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme wa msongo wa 220kV kuanzia Benako hadi Kyaka (Usd 105.4m).
Katika Mazungumzo hayo, Dkt. Nchemba aligusia utekelezaji wa miradi mingine mikubwa ya kimkakati inayoendelea nchini Tanzania ukiwemo mradi wa Reli ya Kisasa SGR, ambao alisema utakapokamilika utakuwa kichocheo kikubwa cha biashara na Uchumi katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Kwa upande wao. Waziri wa Viwanda na Biashasra, Mhe. Dkt. Selemani jafo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzaibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, walisema kuwa ushiriki wa Mfuko wa wa Maendeleo wa Saudi Arabia katika ujenzi wa miradi ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania utachochea maendeleo ya nchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Fund, Bw. Bw. Siultan Al-Marshad, alisema kuwa Mfuko huo uko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania kutokana na uhusiano imara uliopo kwa faida ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Alipongeza hatua kubwa zinazochukuliwa na Serikali katika kutekeleza miradi muhimu kwa maendeleo ya nchi akiitaja Reli ya Kisasa inayojengwa kwamba itachochea na kukuza biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo katika eneo la mradi.
Katika kikao hicho Tanzania na Saudi Fund walikubaliana kuunda Timu ya wataalam watakaopitia, kuchambua na kuchakata miradi mbalimbali ambayo Mfuko huo utatoa fedha ili kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia.
No comments:
Post a Comment