Kwa wale ambao hawakuweza kujishinda kwa siku ya leo naomba niwafahamishe kuwa sisi zote tumekuwa ni washindi. Kushiriki kwenye promosheni yetu tayari tumekuwa washindi na naomba nichukie fursa hii niwajulishe ya kwamba sisi Bakers tutaendelea kuja na promosheni zaidi kwa ajili ya wanafunzi wetu.
Alitaja Shule za Msingi ambazo zilizoibuka washindi kuwa ni Shule ya Msingi Mbezi Beach iliyojinyakulia kompyuta tatu na kompyuta mpakato moja (Laptop), Shule ya Msingi Misewe iliyojishindia kompyuta mbili na kompyuta mpakato moja (Laptop) huku Shule ya Msingi Kigamboni ikiwa ya tatu na kushindia kompyuta moja na Laptop moja.
Wanafunzi watano bora walioshinda Baiskeli za kisasa ni Hassan Musin kutoka shule ya Msingi Mbezi Beach, Marcus Jacob Urasa kutoka shule ya msingi ya Mgulani, James Joseph na Gloria Dickson kutoka shule ya msingi Jaica na Bakary Salum kutoka shule ya msingi ya Amani. Wanafunzi wengine 25 waliweza kujishindia mabegi ya shule.
‘Naomba nitumie fursa hii kuhimiza shule ambazo zimeshinda kompyuta na kompyuta mpakato kuzitumia ipasavyo katika kukuza ujifunzaji wa kidijitali katika shule zao. Sote tunaelewa jinsi ujifunzaji wa kidijitali umekuwa muhimu sana katika shule zetu kwani huwasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa kidijitali katika umri wao mdogo. Aidha itasaidia walimu katika kurahisisha kuzalisha nyenzo za kufundishia na kutoa mbinu mpya za kufundishia, alisema.
Akizungumza kwa niaba ya shule zilizoshinda, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbezi Beach Prisca Haule aliipongeza kampuni ya Bakers Ltd kwa kuja na promosheni ya Kusanya na Ushinde na Bakers akisema kuwa imesaidia kuboresha mazingira yao ya kufundishia kwani pamoja na Kompyuta na Laptops walioshinda zitakuza mbinu zao za ufundishaji.
Promosheni ya Kusanya na Ushinde na Bakers iliweza kufikia shule za msingi 40 jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi walipata fursa adimu ya kujishindia baiskeli za kisasa pamoja na mabegi ya shule huku shule zao zikishinda Kompyuta pamoja na kompyuta mpakato (Laptop).
No comments:
Post a Comment