Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 4 November 2024

KAMPUNI YA BIA YA SBL YATAKA MAZINGIRA YENYE USAWA WA KODI KWENYE BIA

Mhe. Exaud S. Kigahe, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) ambao miongoni mwao ni Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya SBL.
Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara, Mhe. Deodatus Mwanyika akitoa maelezo wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hio kwenye kiwanda cha Serengeti Breweries Limited (SBL) kilichopo Chang'ombe mkoani Dar es Salaam siku ya jumapili, 3 Novemba 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Obinna Anyalebechi akizungumza na Kamati ya Viwanda na Biashara (hawapo pichani) walipofanya ziara ya kikazi kwenye kiwanda hicho kilichopo Chang'ombe mkoani Dar es Salaam siku ya jumapili, 3 Novemba 2024.

Dar es Salaam, November 4, 2024. Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) waishauri serikali kuzingatia kuimairsha mazingira wezeshi ya sera na kodi ili kukuza mapato ya serikali na ukomavu wa biashara nchini. SBL waliyasema haya kwenye kikao na kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara wikiendi hii.


"Hali ya kodi isiyotabirika au yenye upendeleo kwa mzalishaji mmoja inakwamisha ukuaji wa sekta na ukusanyaji wa mapato ya serikali," alisema Mkurugenzi Mkuu wa SBL Obinna Anyalebechi, akitaja punguzo la kodi ya ushuru la 620/- kwa lita kwenye bia inayotengenezwa kutoka shayiri ya ndani kama mojawapo ya kodi zinazobagua.


Punguzo hili la ushuru linaacha pengo la ushuru wa 32% ikilinganishwa na bia inayotengenezwa kutoka shayiri inayoagizwa kutoka nje, ambayo inatozwa ushuru wa 918/- kwa lita, huku watengenezaji wa bia wanaoagiza kutoka nje wakikabiliwa na gharama za ziada za kulipia ushuru wa uagizaji na athari za mabadiliko ya thamani ya fedha za kigeni.


Kwa sasa ni mzalishaji mmoja pekee anayefurahia kodi ya ushuru wa chini kwa bia inayotengenezwa kutoka shayiri ya ndani, na kuwaacha wazalishaji wengine wawili wa bia wenye uwezo mdogo wa uzalishaji – SBL na East African Spirits Limited – wakiwa katika hali isiyofaa kwa kulipa kiwango cha juu cha ushuru wa 918/- kwa lita. “Kiwango chetu kidogo cha uzalishaji wa bia hakiwezi kuhalalisha uwekezaji katika kiwanda cha kutengeneza shayiri kwa sasa,” alisema Obinna, akihimiza kuanzishwa kwa kiwango cha kati cha ushuru cha 680/- kwa lita kwa bia inayotengenezwa kwa kutumia malighafi za ndani kwa 75%.


SBL wameelezea hofu yao kuhusu kodi ya juu inayotozwa kwa shayiri inayoagizwa kutoka nje, na kampuni hiyo imehimiza kamati ivunje muundo huu wa kodi usio na uwiano ili kuimarisha mazingira ya ushindani wa biashara.


SBL ilionya kuwa kodi hizi za ziada zinaweza sio tu kukwamisha ongezeko la mapato, bali pia kusababisha athari zisizotarajiwa katika sekta ya pombe, kama vile ongezeko la bei na kuongezeka kwa uzalishaji wa bia haramu. Kampuni hiyo ilisisitiza kuwa kuhamasisha matumizi ya malighafi za ndani na kuunga mkono kilimo, badala ya kuongeza kodi, kungeleta ongezeko endelevu la mapato hadi shilingi bilioni 71.8 za Kitanzania huku ikilinda sekta ya pombe na uwezo wa walaji kumudu bidhaa.


Mwenyekiti wa Kamati Mh. Deodatus Mwanyika alisema, "Ziara yetu SBL ni moja wapo ya hatua katika kuelewa na kuunga mkono juhudi na malengo mapana ya Tanzania katika maendeleo ya viwanda na biashara. Maarifa tuliyopata kutokana na mazungumzo haya yatasaidia sana katika kuendesha sera zinazowezesha ukuaji wa mapato, kukuza uzalishaji wa ndani, na kuboresha uchumi kwa ujumla."

Kamati hio inatarajia kukutana na wadau tena kutoa muongozo ili kuhakikisha mazingira yanayofaa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya ndani, ambayo yatawezesha mabadiliko ya kiuchumi ya Tanzania na kusaidia kujenga uchumi wa kujitegemea na wenye ustahimilivu.

No comments:

Post a Comment