Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 26 September 2024

EQUITY NA BAKHRESA KUWEZESHA WAFANYABIASHARA KUPATA MIKOPO KIDIGITALI


Benki ya Equity imesema wafanyabiashara ambao wanatumia bidhaa za kampuni ya Bakhresa kwa sasa wana uwezo Equity na Bakhresa kuwezesha wafanyabiashara kupata mikopo kidigitali bidhaa hiyo hadi zaidi ya Shilingi Milioni 300.


Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Equity, Leah Ayoub amesema makubaliano hayo yalianza 2021.


“Tunajua wasambazaji na wajasiriamali wengi wanapata mitaji na kupata changamoto ya riba tukaona turahisishe huduma zetu kwa wateja na wasambazaji wa Azam.


“Tumeingia makubaliano kati ya Benki ya Equity na kampuni ya Bakhresa yenye lengo la kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wa unga. Mfanyabiashara atakuwa na uwezo wa kukopa fedha kwa ajili ya kuota bidhaa hiyo mpaka zaidi ya Shilingi Milioni 300,” amesema.


Amesema lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wanakuza mitaji ambapo kama benki wanatamani wateja hao wakope zaidi ya Shilingi Milioni 300.


Amesema mkopo huo hautakuwa na riba isipokuwa mteja atalipa kamisheni ya kuanzia asilimia 0.5 mpaka 1.5 ambapo mkopaji atapaswa kulipa fedha hizo kuanzia siku saba hadi 30.


“Hii ni fursa ya kukuza mtaji wako kwa haraka. Tumeamua kujitoa kwa wajasiriamali na kuwawezesha wapate huduma kwa urahisi bila vikwazo vingi ambapo mteja hata kama hana akaunti ya Equity ana uwezo wa kuifungua kiganjani mwake akapata mkopo,” amesema Leah.


Naye Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bakhresa Group, Hussein Sufiani amesema makubalino haya yatamsaidia mteja ambapo badala ya kuhangaika kutafuta mfadhili au mdhamini wakumpatia fedha anaweza kwenda benki au kutumia mtandao kupata huduma.

“Hii nayo ni kidigitali, utapata huduma hiyo kwa mfumo wa sms (ujumbe mfupi), sio lazima uende benki kufanya transfer (kuhamisha). Inafanyika moja kwa moja ukishafanya oda yako, kadri unavyozidi kukopa kiwango kinakua,” amesema Sufiani.

Amesema huduma hiyo itawasaidia zaidi wateja wao hasa wadogo hivyo amewahimiza kuchangamkia fursa hiyo.

No comments:

Post a Comment