“Nitumie fursa hii kuwapongeza washindi wetu wote waliotangulia na zaidi pia niwapongeze washindi wa droo yetu kubwa tuliyoifanya hii leo. Kama tulivyobainisha hapo awali Bw Geofrey Muganyizi ambaye ni mshindi wa kwanza atapata gari jipya aina ya Mazda Cx 5 ambapo itakuwa imwekwa mafuta full tank pamoja na bima kubwa ya mwaka mzima buree. Mshindi wa pili, Irene Dominick yeye atapata Bajaj aina ya TVS, na mshindi wa tatu Bhavesh Gorecha atapata pikipiki aina ya Boxer BMX. Zote zikiwa na mafuta pamoja na bima kubwa kwa mwaka mzima’’ alisema.
Akizungumzia zaidi mafanikio ya kampeni hiyo, Bw. Stanley Kafu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Exim, alisema “Kampeni ya Tap Tap Utoboe imekuwa na matokeo mazuri katika kuongeza uelewa na matumizi ya huduma zetu za kidijitali. Tumefurahi kuwa wateja wetu wengi wamevutiwa na huduma hii na hili limedhihilishwa na ongezeko la miamala ya kidijitali tangu kampeni hii ianze mpaka sasa hivi”.
“Dhumuni kuu ni kuhakikisha mteja wetu anapata huduma zenye ubora, kwa wakati popote alipo kwa gharama nafuu,” aliongeza Stanley.
Naye Silas Matoi, Mkuu wa Njia Mbadala za Kidijitali wa Exim Bank, alielezea umuhimu wa ubunifu wa kidijitali kwa benki hiyo. “Ubunifu wa kidijitali ndio kiini cha mkakati wetu wa kuboresha huduma zetu kwa wateja. Kampeni ya Tap Tap Utoboe imeonesha jinsi teknolojia inavyoweza kubadilisha namna ambavyo wateja wetu wanatumia huduma za kifedha. Tumewavutia wateja wapya na wa zamani kwa kuwapa fursa ya kushinda zawadi, huku tukiunga mkono ajenda yetu ya kuendeleza uchumi wa kidijitali,” alisema Silas.
Kampeni ya Tap Tap Utoboe ilikuwa sehemu ya jitihada za Benki ya Exim kuhimiza jamii kufanya miamala kwa njia za kielectroniki, ikiwemo kupitia simu za mkononi na mtandao, sambamba na malengo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya kuimarisha matumizi ya mfumo wa kifedha wa kidijitali.
No comments:
Post a Comment