Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 2 July 2024

TAFINA WATANGAZA UJIO WA KONGAMANO KUBWA LA UWEKEZAJI AFRIKA MASHARIKI (EAIF) 2024


Dar es Salaam, Tanzania - Julai 01, 2024 – Chama cha Fintech Tanzania (TAFINA) kinafuraha kutangaza Ujio wa Kongamano la Uwekezaji la Afrika Mashariki (EAIF) 2024, tukio la kihistoria ambalo litabadilisha hali ya teknolojia ya Afrika Mashariki. Kongamano hili, lililoandaliwa kwa ushirikiano na vyama vikuu vya fintech kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Tanzania, litafanyika Septemba 12 na 13, 2024, katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Tanzania.

EAIF 2024 ni tukio la siku mbili linalotayarishwa kuwa na mkusanyiko muhimu wa wadau wakuu katika sekta ya fintech. Inalenga kuchunguza na kujadili hali ya teknolojia ya kifedha inayobadilika na inayoendelea kwa kasi ndani ya Afrika Mashariki. Kwa kuzingatia uvumbuzi, uwekezaji na ushirikiano, kongamano hili linalenga kuwezesha mijadala muhimu , kuhimiza ushirikiano wa kimkakati, na kuvutia uwekezaji mkubwa katika eneo hili.

“Tunafuraha kubwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hili la Uwekezaji la Afrika Mashariki. Mada kuu ya kongamano hili ni " Invest & Partner : Leave No One Behind " Tunatumai kuwa kongamano hili litakuwa na mazungumzo ya maana na ushirikiano wa kimkakati, ubia na uwekezaji ndani ya mfumo ikolojia wa Fintech wa Afrika Mashariki,” alisema Cynthia Ponera, Mwenyekiti wa TAFINA.

Mwaka huu tupo na Selcom Tanzania, mdau wetu wa TAFINA ambaye ataratibu mfumo mzima wa malipo kuelekea kongamano hili ," aliongezea

Kwa upande wao Selcom

"Tunajivunia kuunganisha nguvu na TAFINA kwa ajili ya Jukwaa la Uwekezaji la Afrika Mashariki, tutatoa lango la malipo bila usumbufu kwa kila anayepanga kuhudhuria kongamano hili kupitia tovuti ya TAFINA – Shumbana Walwa, Mkuu wa Masoko wa Selcom Tanzania

EAIF 2024 itakua na matukio mazuri na ya kusisimua ikiwemo mada mbalimbali zitaendeshwa, mijadala ya jopo, na vikao vya mitandao na viongozi wa sekta, wawekezaji, watunga sera, na wavumbuzi.

Wahudhuriaji watakuwa na nafasi ya kujihusisha na teknolojia za kisasa, kuchunguza fursa za uwekezaji, na kushirikiana katika kutatua changamoto kubwa za kifedha za kanda.

Ili kujua zaidi kuhusu tukio au kujiandikisha, wadau na wahusika watembelee

https://tafina.or.tz/east-africa-investment-forum-eaif/

No comments:

Post a Comment