Foreign Exchange Rates

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

Wednesday, 14 February 2024

MGAHAWA WA KFC WAFUNGUA TAWI ARUSHA


Katika kuhakikisha watanzania pamoja na wageni wengine wanaofika hapa nchini kutalii wanapata huduma bora ya chakula, Mgahawa wa KFC umefungua tawi Jijini Arusha.


Tawi hilo linakuwa la tisa kufunguliwa hapa nchini tangu mgahawa huo wa kimataifa wenye Makao yake makuu nchini Marekani kufungua tawi lake la kwanza Jijini Dar es Salaam mwaka 2013. Kampuni ya Dough Works Limited ni mbia wa hapa nchini wa KFC pia inasimamia Piza Hut pamoja na Bao Café huduma ya chakula inayokua kwa kasi nchini.


Akizungumzia kuhusiana na uamuzi wa kufungua KFC Jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Dough Works, Vikram Desai amebainisha kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa Tanzania kwa kuwa mbali na kuwafikishia wananchi huduma bora ya chakula lakini pia inachangia ajira kwa watanzania.


Amesema, Arusha ni Jiji la kitalii ambapo watalii wamekuwa wakifika kwa wingi kutalii, hivyo kwa uwepo wa KFC Arusha itawapatia huduma za chakula chenye hadhi ya kimataifa.


Alisema, "leo ni siku nzuri kwetu kampuni ya Dough Works kwa kuwa tunaungana na serikali katika kuimarisha huduma kwa watalii, huu mgahawa wa KFC ni wa kimataifa na upo kwenye nchi zaidi ya 140 hivyo watalii wakifika Arusha na kukuta kuna KFC kama kati ya huduma za chakula wanafurahi zaidi.”


Amesema kwa hapa nchini Migahawa ya KFC inapatikana Mlimani City Mall, Masaki, Diamond Plaza –City Center, Mikocheni Plaza, Kariakoo, Morocco, Mbezi Beach na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


Alisema kuwa baada ya kufungua tawi la Arusha itafuata zamu ya Dodoma na Zanzibar.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Energies Tanzania, Kalpesh Mehta amesema kuwa kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha inashirikiana na kampuni ya Dough Works Tanzania katika kuhakikisha huduma ya KFC inatolewa kwa ufanisi hapa Arusha.


“Kwa kuwa hapa katika ORYX kuna huduma mbalimbali mbadala zinazoendana na huduma za magari ikiwemo service za magari au uoshaji wake pamoja na huduma nyinginem kwetu kufanya kazi na Dough Works katika biashara ya KFC tutawafikia wateja wengi zaidi” alisema Mehta.

No comments:

Post a Comment