| Mshindi wa pesa taslimu shilingi milioni 10 kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, Bw. Maduhu Sayi Msekwa (kulia) akiwa ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Masta Shangwe katika viwanja vya Machinga Complex jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo. |
No comments:
Post a Comment