Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Tuesday, 17 October 2023

WATEJA WA STANCHART KUPATA HUDUMA KUPITIA TCB BANK

Benki ya Standard Chartered Tanzania (SCB) iliandaa hafla ya kuamsha kinywa kwa wateja wake wa Biashara katika Hoteli ya Hyatt Regency ikiwa pamoja na Benki ya Biashara Tanzania lengo ikiwa ni kuhamasisha huduma inayowawezesha wateja wa Standard Chartered Bank kutumia mtandao wa TCB kuweka na kutoa pesa kwenye Matawi yake 82 pamoja na Wakala 5,600 wa TCB kote nchini.

Ushirikiano huu unalenga kutoa urahisi, wakati halisi na mazingira salama kwa wateja wa Standared Chartered Bank kutekeleza huduma zao za benki.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Bw. Jema Msuya pamoja na wawakilishi waandamizi kutoka benki hiyo, Rayson Foya, pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Standared Chartered ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala, Efeh Amoah pamoja na maafisa wengine kutoka SCB.

No comments:

Post a Comment