Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 6 July 2021

BENKI YA TPB YAKABIDHI MAJENGO YA VYOO SHULE YA MSINGI IFWAGI – MUFINDI

Majengo mapya ya vyoo vya Shule ya Msingi Ifwagi Wilayani Mufindi, Mkoani Iringa.
Wafanyakazi wa Benki ya TPB kwenye picha ya pamoja.
Picha ya pamoja uongozi wa Benki ya TPB na wanafunzi.

Benki ya TPB imesaidia kuondoa changamoto ya vyoo kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Ifwagi iliyopo katika kijiji cha Ifwagi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Hayo yalibainishwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bi Imani Nyoni wakati alipokuwa akisoma risala ya shule yake kwenye hafla ya kukabidhiwa majengo yenye matundu 20 ya vyoo kutoka Benki ya TPB yaliyokabidhiwa shuleni hapo.

Nyoni aliwashukuru TPB kwa kuwaondolea changamoto ya uhababa wa majengo ya vyoo yaliyokuwa kwenye hali isiyoridhisha na mengine kutoka kutumika kabisa ambayo yalisababisha athari kubwa kiafya kwa wanafunzi pamoja na walimu.

“Shule yetu ya Ifwagi ina wanafunzi wasiopungua 211 ambao wote walikuwa wanategemea matundu machache sana ya vyoo wakati wakiwa shuleni”, alisema.

Alibainisha kuwa shule hiyo kwa muda wa kipindi kirefu walikuwa wakijaribu kuomba wafadhili mbalimbali kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa majengo mapya ya wanafunzi pamoja na walimu pasipokupata mafanikio.

Kadhalika alisema ilibidi bodi ya shule iweze kufanya kikao na wazazi, walezi pamoja na wanakijiji mbalimbali waweze kununu vifaa mbalimbali vya ujenzi ili wajenge kwa nguvu zao wenyewe. Katikati ya mchakato huo ndio tukapata wafadhili wetu kutoka benki ya TPB ambao ki ukweli ni wadau wakubwa sana kwenye elimu na waliweza kusaidia hadi leo hii tupo hapa tunakabidhiwa majengo haya.

Aidha alizitaja changamoto nyingi kuwa ni uhaba wa maji katika shule ya ifwagi ambapo inawalazimu wanafunzi kwenda kufata maji kwa umbali mrefu sana kwa ajili ya kusaidia kuendesha shughuli mbalimbali shuleni.

Naye Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa Benki ya TPB kutoka Makao Makuu, Bi Diana Myonga akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa majengo hayo alisema TPB imekabidhi majengo ya matundu 20 ya vyoo yenye thamani ya sh milioni hamsini na sita na laki mbili kwa ajili ya shule ya Msingi Ifwagi.

Myonga aliongeza kuwa pia TPB watatota msaada wa samani za ofisi za walimu ambazo waliomba shule kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi shuleni hapo.

Alisema msaada huo ni sehemu ya TPB kurudisha faida kwenye hamii kutokana na kuiunga mkono benki hiyo.

Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo TPBB wamekuwa wakitoa msaada kuwa ni sekta ya afya kwa kutoa vifaa tiba, mashuka magodoro na sekta ya elimu ambapo husaidia kutoa madawati, viti, meza na kuchangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya shule na vituo vya afya.

Alimaliza kwa kutoa rai kwa wanafunzi pamoja na walimu kuwa wayatunze majengo hayo ili yaweza kukaa kwa muda mrefu na kusaidia watoto wengine huko mbeleni. Aliongeza kwa kukaribisha wananchi wote wa kijiji cha Ifwagi na maeneo ya karibu kukaribia katika tawi la TPB lililopo Mafinga mjini kwa ajili ya kujipatia huduma mbalimbali za kibenki kwa gharama nafuu.

Kwa Mawasiliano Zaidi:-

Chichi Banda
Kaimu Meneja Mwandamizi wa Mwasiliano na Uhusiano
Benki ya TPB
0682 136414

No comments:

Post a Comment