Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 19 October 2020

BENKI YA DCB YATOA GAWIO KWA WANAHISA WAKE WAKUU

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo, akikabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya shilingi 138,603,889 ikiwa ni gawio la wanahisa kutoka Benki ya DCB kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Zawadia Nanyaro, hafla hiyo imefanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe; Selemani Jafo (wa tatu kushoto), akikabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya shilingi 30,780,000 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga ikiwa ni gawio la hisa za shirika hilo kutoka Benki ya DCB. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Zawadia Nanyaro, hafla hiyo imefanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, akiwakaribisha Mkuu Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri na Mkurugenzi wa Jiji Bi Sipora Jonathan wakati wa hafla ya Benki ya DCB ilipokuwa ikitoa Gawio kwa wanahisa wake wakuu jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Uwekezaji (UTT) Simon Migangala wakati wa hafla ya benki ya DCB ya kutoa gawio kwa wanahisa wake wakuu jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Zawadia Nanyaro.

No comments:

Post a Comment