Nsekela alisema katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na ugonjwa wa Corona hakunabudi kwa taasisi na mashirika yote kuungana na Serikali na wataalamu wa afya katika kutoa elimu kwa Watanzania itakayosaidia kupunguza maambukizi na kuondokana kabisa na ugonjwa huo wa Corona.
“Benki yetu ya CRDB tayari imeshachukua hatua mbalimbali zinazosaidia kuwakinga wafanyakazi na wateja wetu, ikiwamo kuweka dawa za kusafisha mikono (hand sanitizer) katika ofisi zetu, matawi pamoja na ATM,” alisema Nsekela huku akishukuru Wizara ya Afya na Chama cha Madaktari kwa kuwa nao bega kwa bega katika kutoa elimu kwa wafanyakazi na wateja wa benki hiyo.
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Elisha Osati, akinawa mikono ikiwa ni tahadhari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona. |
"Tunaagana" |
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na wateja wa Tawi la Azikiwe jijini Dar es Salaam. |
“Wajibu wetu nikuhakikisha madaktari, wauguzi na watumishi wote wa sekta ya afya wanakuwa na elimu ya kutosha ya kupambana na ugonjwa huu. Tukiweza kuwafikia hawa itasaidia elimu hii kusambaa kwa Wananchi wengi na hivyo kuepukana kabisa na ugonjwa huu wa Corona,” alisema Dkt. Osati huku akiwataka na wadau wengine kuungana Benki ya CRDB.
Hafla hiyo pia iliambatana na zoezi la uhamasishaji wa kunawa mikono kwa wananchi ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa kushirikiana na Raisi wa Chama cha Madaktari, Dkt. Elisha Osati na Katibu wa cha hicho, Dkt. Lilian Mnabwiru waliochesha namna bora ya kunawa mikono, huku wakiwahamasisha Watanzania kunawa mikono mara kwa mara ikiwa ni njia ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.
“Katika mapambano na ugonjwa huu wa Corona zoezi la kunawa mikono ni muhimu sana, tumekuwa tukiwahimisha wafanyakazi na wateja wetu, na sasa tunaungana na Chama cha Madaktari kuwahamasisha Watanzania kunawa mikono mara kwa mara au kutumia vitakasa mikono (hand sanitizer),” alisema Nsekela huku akimtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya TTCL, Waziri Kindamba kuungana naye kuwahamasisha Watanzania kunawa mikono katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.
No comments:
Post a Comment