Pamoja na changamoto iliyopo duniani kwa sasa, MultiChoice inawahakikishia wateja wake wa DStv kuwa inayazingatia mahitaji yao has ukizingatia kuwa kwa sasa watu wengi wanalazimika kukaa nyumbani katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
“Tutaendelea kukupa wigo mpana zaidi wa kupata habari za uhakika kwa kufungua chaneli za habari kwenye vifurushi vyetu. Tunazingatia mawasiliano ya mara kwa mara na mamlaka husika na tutashiriki kikamilifu katika kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa Covid-19. Ni muhimu sana sote tuzingatie maelekezo na maagizo yanayotolewa na mamlaka sahihi na wataalamu wetu ili kuhakikisha kuwa tunalinda afya zetu na za wenzetu” amesema Jacqueline Woiso, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania
Mkurugenzi huyo ametangaza rasmi kwamba kuanzia sasa;
- Fahamu kinachoendelea
- Kwa watoto
- Michezo
Huduma kwa wateja:
Tunajali afya za wateja na wafanyakazi wetu, katika kipindi hiki cha tahadhari tumeandaa utaratibu ambapo baadhi ya wafanyakazi watafanya kazi wakiwa nyumbani. Hii ina maana kuwa kunaweza kukawa na kuchelewa kupata huduma. Hata hivyo tuna njia nyingi mbadala za kidijitali - kimtandao ambapo mteja anaweza kupata huduma nyingi kwa urahisi na ufanisi zaidi.
Huduma hizo ni pamoja na ; My DStv App inayopatikana kwenye Google Play na App Store, IVR – huduma ya sauti iliyorekodiwa, Huduma ya WhatsApp kwa namba 0677 666 111 ambapo unaweza kufanya malipo, kubadili kifurushi, kuangalia salio na huduma nyingine muhimu. Pia unaweza kupiga simu Huduma kwa wateja kupitia namba +255 222 199600 na +255 784 104 700, Tovuti : www.dstv.com, USSD: *150*53# pamoja na huduma ya ujumbe mfupi SMS kwenda 15727
Kwa wewe unayetaka kufungiwa huduma ya DStv wakati huu, fahamu kuwa mafundi wetu wote wamechukua tahadhari kubwa kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa usalama. Mafundi wamepewa mahitaji muhimu na maelekezo rasmi ya kuchukua tahadhari wakati wa kutoa huduma.
Mabadiliko ya ratiba
Kutokana na hali hii ya dharura, michezo mingi imeathirika. Athari hizi pia zimezikumba tasnia nyingine za michezo na burudani kama vile uzalishaji wa filamu. Tutakuwa tukiwajuza wateja wetu kuhusu mabadiliko ya ratiba kadiri yatakavyokuwa yanatokea. Pi unaweza kutembelea www.dstv.com
No comments:
Post a Comment