Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 19 July 2019

BENKI YA NBC YATOA SHILINGI BILIONI 2.1 KUKOPESHA WASTAAFU

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Venance Mashiba (wa pili kulia), na Mkurugenzi Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa (kulia kwake), wakikata keki kusherehekea uzinduzi rasmi tawi jipya la Benki ya NBC Tegeta katika jengo la Kibo Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Kitengo cha Makampuni, Linley Kapya, Mnadhimu Mkuu Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Joyce Mbago, Meneja wa Tawi la Tegeta, Edward Chibombo na Mkurugenzi wa Fedha, Waziri Barnabas.
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Venance Mashiba ( wa nne kushoto), na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa (kushoto kwake), wakikata utepe kuzindua rasmi tawi jipya la Benki ya NBC Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Kitengo cha Makampuni, Linley Kapya, Mnadhimu Mkuu Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Joyce Mbago, Mkurugenzi wa Fedha, Waziri Barnabas na Meneja wa Tawi la Tegeta, Edward Chibombo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la benki hiyo la Tegeta katika jengo la Kibo Complex jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Gaudence Shawa (katikati waliokaa) Mkurugenzi wa Kitengo cha Makampuni, Linley Kapya (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Fedha, Waziri Barnabas (kushoto kwake), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi katika tawi hilo na baadhi ya maofisa wa NBC katika hafla hiyo.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) nchini imetoa mikopo yenye jumla ya kiasi cha shilingi Billioni 2.1 kwa wastaafu tokea ilipozindua huduma ya mikopo ya wastaafu Juni mwaka jana.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Theobald Sabi, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bw Gaudence Shawa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Benki hiyo la Tegeta Kibo Commercial Complex alisema kwamba benki hiyo imewatambua wastaafu kama kundi muhimu la kiuchumi.

“NBC tumewatambua wastaafu wanaopokea pensheni kama kundi la kiuchumi ambalo lina uwezo wa kuchangia katika uchumi wa taifa letu kwa kuwezeshwa kifedha,”

“Kikwazo kikubwa, kwa siku za huko nyuma, ilikuwa kutokuwepo kwa bima ya mikopo kwa watu waliovuka umri wa miaka 60, sasa ipo bima inayowakinga wastaafu waliovuka umri huo hapa nchini,” aliongeza alipozungumza na wageni waalikwa jana kwenye hafla ya uzindi.

Alifafanua kwamba kwa kutambua umuhimu wa wafanyabiashara wadogo na wakati, mnamo mwaka 2016, uongozi wa benki hiyo uliunda kurugenzi maalum ya kuhudumia wateja hao na hadi mwezi machi mwaka huu benki hiyo imeshatoa jumla Tsh 155 billioni kama mikopo kwa wafanyabiashara 3,000 nchini.

Aliongeza kwamba benki hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) ambayo Benki tanzu ya Benki ya Dunia imefanya mapitio ya kina ya utaratibu mzima wa utoaji wa mikopo katika kundi hilo ili waweze kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.

Bw Shawa alifafanua kwamba kupitia hotuba ya mkurugenzi mtendaji alisema benki hiyo imewawezesha wateja binafsi takribani 27,000 kwa mikopo isiyokuwa na dhamana yenye thamani Tsh 337,000 kati ya hao 53% ni watumishi wa serikali na 47% ni kutoka sekta binafsi.

“Azma ya benki hii ni kuwakuza wafanyabishara wadogo hadi wafikie hatua ya kuchangia katika uchumi wa Tanzania na katika kutimiza lengo hilo benki hii imezindua klabu za biashara zijulikanazo kama ‘Business Clubs” katika mikoa mbali mbali nchini,” alisema.

Alisema kwamba dhumuni la kuanzisha Klabu hizo ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara hao kwa mafunzo maalum ya kuendesha biashara zao kwa njia ya kisasa na kuongeza uzalishaji, faida na tija ya uendeshaji.

Bw Shawa aliongeza kwamba mafunzo hayo yanaratibiwa na benki hiyo kwa kushirikiana na taasisi kadhaa kama vile Mamlaka ya Biashra Tanzania, Kituo cha Uwekezaji (TIC), Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO), Chama cha wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pamoja na mambo mengine hadi kufikia disemba mwaka jana benki hiyo ilikuwa imetoa mafunzo hayo kwa takribani wafanyabiashara 7,000 na lengo ni kuwafikia zaidi ya 1,000.

Aliongeza kwamba benki hiyo ni mojawapo wa benki hapa nchini iliyojiunga na mfumo wa Kukusanya Fedha za Umma (GePG) mwaka jana na hadi kufikia disemba 2018, ilikuwa imekusanya maduhuli ya serikali Tsh 201 billioni ikionyesha ukusanyaji wa wastani Tsh 16 billioni kwa mwezi.

Benki hiyo ni moja ya taasisis za fedha kongwe nchini iliyoanzishwa kwa sheria namba 1 ya 1967 iliyopitishwa na bunge la Tanzania kwa lengo la kupeleka huduma za kibenki kwa watanzania na hivyo kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi.

No comments:

Post a Comment