Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 30 April 2019

WHATSAPP KUTUMIKA KUWAHUDUMIA WATEJA WA TIGO

Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo Mwangaza Matotola, akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ambavyo huduma ya WhatsApp inavyoweza kutumiwa na mteja kuuliza au kupata ufafanuzi kutoka kwa watoa huduma wa Tigo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisael.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisael (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya WhatsApp ambayo inaweza kutumiwa na wateja wa kampuni hiyo kuuliza au kupata ufafanuzi wa bidhaa na huduma mbali mbali za kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Tigo Mwangaza Matotola.
Kampuni ya Tigo Tanzania, imezindua huduma ya whatsApp kwa ajili ya kuwahudumia wateja wake.

Huduma hii ya kidijitali, itawawezesha wateja wa Tigo kutuma dukuduku zao na kupokea majibu ya papo kwa papo watakapotumia namba ya WhatsApp ambayo ni 0675100100.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Tigo Mwangaza Matotola alisema, Tigo imekuwa kampuni ya kwanza nchini kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kuwahudumia wateja wake.

“Kupitia huduma hii mpya, wateja wa Tigo watapata uzoefu binafsi pamoja na kupata majibu ya papo kwa papo watapotaka kupata ufafanuzi wa jambo au utatuzi wa changamoto zozote katika kutuia mtandao wetu,” alisema

WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii yenye nguvu sana duniani kwa sasa. “Kwa kuzingatia ukweli huu, huduma hii itawawezesha wateja wa Tigo kupata huduma binafsi na zenye usalama. Uzinduzi wa huduma hii ni moja kati ya mikakati yetu ya kuhamasisha maisha ya kidijitali, vile vile tunapanua wigo wa namna wateja wetu wanavyoweza kuhudumiwa tunavyoongeza WhatsApp kwenye huduma zetu za mitandaoa ya kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter. Huduma ya WhatsApp inapitakana kwa wateja wote wa Tigo,” alifafanua Mwangaza.

Mwangaza aliongeza kuwa, huduma hiyo imetengenezwa maalum kwa ajili ya kumhudumia mtu mmoja mmoja na siyo kuwahudumai watu kwa pamoja kama kundi (group la WhatsApp). “Mteja siyo tu ataweza kujielezea kupitia huduma hii lakini pia anaweza kutuma picha kwenye mfumo wa ‘screenshot’ kwenda namba 0675100100 na atapata majibu ya papo kwa papo kwa kile atachoakiuliza au kutaka ufafanunuzi/utatuzi,” alisema.

“Tigo Tanzania inajivunia kuwa kampuni ya simu namba moja kwenye mageuzi ya kidijitali pamoja na uvumbuzi. Tigo imeweza kuwa ya kwanza kuzindua bidhaa nyingi kwenye soko la Tanzania ambazo zinathibitisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora kwa wateja wetu pamoja na uzoefu wa aina yake. huduma hii ya WhatsApp ni sehemu ya safari yetu hii ya mageuzi ya kidijitali,” aliongeza

Wateja wanaotumia WhatsApp wanaweza kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja cha Tigo muda wowote wanaopenda na kama itatokea kukawa na kuchelewa kupata mrejesho atapokea ujumbe mfupi.

Huduma hii mpya ya WhatsApp kwa ajili ya kuwahuduma wateja, ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya Tigo kuwapatia wateja wake uzoefu wa aina yake na wa kipekee wa huduma zake kwa njia ya kidijitali na kurahisisha maisha yao ya kila siku kupitia huduma zilizojaa ubunifu.

No comments:

Post a Comment