Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 26 April 2019

KONGAMANO LA KIMATAIFA LA QNET LAWALETA PAMOJA WAJASIRIAMALI 13,000 PENANG


Wageni waheshima wa QNET, Maofisa wa Malaysia na wageni wa heshima waalikwa wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa kongamano la siku tano la QNET lililofanyika jijini nchini Malaysia. Zaidi ya wajasiriamali 13,000 waliudhuria kwenye maonyesho hayo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa QNET na Wageni wa heshima wakiwa wamepozi pamoja mara baada ya kukata utepe wa uzinduzi wa kongamano la siku tano la QNET.
Penang, Tarehe 23 Aprili 2019 - Kampuni maarufu ya kimataifa yenye asili ya Asia ya mauzo ya moja kwa moja, QNET inaendesha kongamano la siku tano la kimataifa ambalo linaleta pamoja takribani wajasiriamali 13,000 kutoka maeneo mbalimbali duniani katika kisiwa cha Penang

Kongamano lenye hamasa litashuhudiwa na wasambazaji wa QNET kutoka katika zaidi ya nchi 30 watakao kutana pamoja katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa na maonyesho wa Subterranean Penang International Conference & Exhibition Centre (SPICE) katika mji wa Bayan Baru, Penang, Malaysia

Shughuli za ufunguzi wa sherehe zilifanywa na Yang Berhormat Profesa Dr. P. Ramasamy, Naibu Waziri Kiongozi II wa Penang, Mwenyekiti Mtendaji wa QI Group, Dato Sri Vijay Eswaran na Kaimu Naibu Mwenyekiti Joseph Bismark. Vile vile walikuwepo Mh. Cissé Ibrahim Sory, Meneja Mkuu wa Guinea Microfinance Agency ANAMIF, na washirika wengine wa biashara za kimataifa wa QNET kutoka Afrika, na sehemu mbalimbali duniani.

Kongamano hili ambalo linajulikana kama V-Malaysia 2019 limefanyika Penang kwa miaka sita mfululizo. Wateja na wasambazaji kutoka katika masoko makubwa ya kikanda ya QNET katika Mashariki ya Kati, Katikati ya Asia, Afrika, Bara Hindi, Indonesia na Malaysia wanahudhuria kongamano la mwaka huu. Kongamano la siku tano litajumuisha mfululizo wa programu za mafunzo, hotuba za uhamasishaji, kutambulisha bidhaa mpya za mtindo wa maisha wa QNET na burudani. Kivutio kikubwa mwaka huu ni QNET Carnival ambayo itaonyesha zaidi ya nembo au lebo 50 za bidhaa za QNET katika moja ya maonyesho makubwa kuwahi kufanywa na kampuni hiyo.

Katika hotuba yake, Naibu Waziri Kiongozi II wa Penang Profesa Dr. P. Ramasamy alitoa shukurani zake kwa QNET kwa kuja Penang kwa miaka sita mfululizo na kufanya kongamano kubwa la siku tano.

"Ningependa kusisitiza kwamba Penang inajulikana vyema kwa ari yake ya ujasiriamali na kwa kutengeneza wajasiriamali kwa miaka mingi nchini. Ninahakika kwamba QNET itasaidia kuhamasisha wajasiriamali wa leo kuwa chombo cha mabadiliko ya kesho," alisema Dr. P. Ramasamy na kufuatia na shangwe za nguvu na makofi kutoka kwa wasambazaji wa QNET kutoka sehemu mbalimbaloi duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa QNET Bwana, Malou Caluza alisema: "Matukio kama haya ya Kongamano - V (V-Convention) linatupa fursa ya kuwahudumia wasambazaji wetu na kuwaruhusu kuwa na sisi kwa karibu. Tumewaleta takribani wafanyakazi 250 kutoka katika maeneo mbalimbali duniani kutusaidia katika kongamano hili na kuwapa washiriki wa kongamano hili uzoefu wa hali ya juu. Vile vile ni jukwaa bora la kusherehekea ari ya ujasiriamali ambayo kampuni ya mauzo ya moja kwa moja kama QNET inachochea kwa mamilioni ya watu duniani kote, kuwasaidia kuboresha maisha yao na kuchangia katika jamii."

Akiongeza katika hilo, Meneja Mkuu wa QNET wa eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara bwana M. Biram Fall alisema: "V - Malaysia inafuatilia kongamano lenye mafanikio 2019 la msimu wa QNET Expo lililokuwa linajulikana kama Absolute Living, sambamba na misingi ya kampuni ya mauzo ya moja kwa moja na falsafa ya RYTHM - Raise Yourself to Help Mankind – inayofanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa na huduma zake zilizoko sokoni ambalo lilianza mwaka 2019 jijini Dar es salaam, Tanzania mwezi uliopita, kisha kuhamia jijini Kumasi, Ghana na baadae katika nchi nyingine za Afrika.

QNET, Kampuni tanzu inayoongoza ya kundi la makampuni la QI (QI Group of Companies), inauza reja reja bidhaa mbalimbali za Afya na ustawi, huduma binafsi na urembo, sikukuu, utunzaji wa nyumba na kozi kwa njia ya mtandao miongoni mwa nyingi zingine ambazo zinaboresha maisha ya kila siku ya wateja wake duniani kote. QNET iliwekwa katika moja kati ya makampuni 100 makubwa na imara ya MLM (Solid Top MLM Companies) kwa mwaka 2018 na Portal ya habari za mauzo ya moja kwa moja ya Business for Home.

Kuhusu QNET

QNET ni moja kati ya makampuni ya mauzo ya moja kwa moja kutoka Asia yanayoongoza ambayo inatoa aina mbalimbali za bidhaa za afya, ustawi na mitindo ya maisha ambayo yanasaidia watu kuishi maisha bora zaidi. Kwa miaka 20, Mtindo wa biashara ya kuanzia ngazi ya chini ya QNET umeongezewa kasi na nguvu ya biashara ya mtandao imesaidia kuwawezesha mamiloni ya wajasiriamali katika nchi zaidi ya 100 duniani kote.

Makao makuu ya QNET yako Hong Kong na imefungua ofisi zake katika zaidi ya nchi 25 duniani kote kupitia kampuni tanzu, ofisi za matawi yake, ushirikishaji wa mawakala na uwakala.

QNET ni mwanachama wa Chama cha wauzaji wa moja kwa moja (Direct Selling Association) cha Malayasia, Singapore, Ufilipino, Indonesia na UAE, pamoja na Chama cha Chakula Bora cha Hong Kong (Hong Kong Health Food Association) na Chama cha viwanda vya Virutubisho vya afya cha Singapore (Health Supplements Industry Association) miongoni wa vingine.

QNET pia inafanya vizuri katika udhamini wa michezo duniani. Baadhi ya ushirikiano maarufu unajumuisha kuwa Mshirika wa moja kwa moja wa mauzo wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester City na klabu ya Ligi ya Mabingwa Afrika (African Club League Championships of CAF) Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya QNET kupitia www.qnet.net na blog ya QNET Africa kupitia www.qnetafrique.com

Mawasiliano kwaajili ya Vyombo vya Habari;

Maxime PETI
Maxime.peti@qnet.net
62(+225) 07054430(2)

No comments:

Post a Comment