Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 20 March 2019

TANZANIA YAPELEKA MSAADA WA CHAKULA NA MADAWA KWA NCHI ZA MALAWI, MSUMBIJI NA ZIMBABWE KUTOKANA NA KUKUMBWA NA MAFURIKO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakiwa na Balozi wa Malawi, Mhe. Glad Chembe Munthali (kushoto), Balozi wa Msumbiji, Mhe. Monica D.C. Mussa (wa pili kushoto) na Balozi Mdogo wa Zimambwe nchini, Mhe. Martin Tavenyika (wa tatu kushoto) wakati wa zoezi la kuwakabidhi mabalozi hao misaada ya dawa na chakula ambavyo Serikali ya Tanzania imetoa kwa nchi zao ambazo zimekumbwa na maafa yaliyosababishwa na mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika. Tukio hilo limefanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi 2019.
Mhe. Prof. Kabudi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhe. Waziri Ummy kuhusu aina ya dawa zilizotolewa msaada kwenye nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kufuatia maafa yaliyosababishwa na mafuriko yaliyozikumba nchi hizo. 
Sehemu ya magari yaliyobeba shehena ya msaada wa dawa na chakula kwa ajili ya waathirika wa mafuriko kwenye nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kama inavyoonekana kabla ya kuanza kupakiwa kwenye ndege.
Askari wa Jeshi la Ulinzi wakishusha kwenye magari na kupakia kwenye ndege misaada ya madawa na chakula ambavyo Serikali ya Tanzania imetoa msaada kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe ambazo zimekumbwa na maafa ya mafuriko kufuatia tufani kali iliyolikumba eneo hilo la kusini mwa Afrika.
Read More >>

No comments:

Post a Comment