Machi 19, 2019 - DTB-Tanzania imeweka historia kwa kuzindua huduma 3 ambazo zitaongeza ufanisi katika jitihada za kuwafikia wateja waliombali na matawi na kupunguza gharama za kupata huduma za kibenki kwa wateja wake. Huduma zilizozinduliwa hivi karibuni ni pamoja na Prepaid Card, DTB wakala na Merchant Payment devices (POS).
Kadi hizi za Pre-Paid ambazo zipo kwenye mfumo wa MasterCard, zina uwezo wa kubeba fedha aina kumi zinazotambulika kimataifa tofauti na Shilingi ya Tanzania ambayo ni fedha namba moja. Hivyo kadi hizi zinafaa kwa wafanyabiashara wanaosafiri nje ya nchi kwa matibabu, wanafunzi wanaosoma nje ya nchi na watalii. Fedha hizi ni pamoja na Dola za kimarekani, Yuro ya bara la Ulaya, Paundi ya Uingerereza, Dirham ya Ufalme za Kiarabu, Rupee ya India, Randi ya Afrika Kusini, Yuan ya Uchina, Dola ya Canada na Shilingi za Kenya na Uganda.
Kadi hizi za Pre-Paid zipo kwenye teknolojia ya hali ya juu ili kuimarisha usalama kwa wateja na haziwezi kughushiwa kwa namna yoyote.
Akizungumza na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi, Mwenyekiti wa Bodi ya DTB- Tanzania Ndg. Abdul Samji Alisema, “Sisi kama benki dhamira yetu ya kuboresha huduma kwa wateja kwa kuwekeza kwenye teknolojia inapewa kipaumbele namba moja. Nina furaha kwamba kwa mara nyengine tunaweletea huduma salama, rahisi na yenye thamani kwa pesa za wateja wetu”.
Ndg. Samji aliongeza “Kwa kuzindua huduma kupitia mawakala, wateja wetu watapata huduma za kibenki moja kwa moja kupitia mawakala 110 ambao wamesambaa nchi nzima. Huduma zinazopatikana kwa kupitis mawakala wetu ni kuweka fedha, kutoa pesa na kuangalia taarifa fupi za miamala.
Huduma za kibenki kupitia mawakala ni mkakati mahususi wa kuongeza ufanisi kiuchumi kwa kufikia watanzania waliopo katika maeneo ambayo hakuna huduma za kibenki ambao ni zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wote. Katika hali hii, huduma kupitia mawakala zinakuwa ni muhimu hasa katika sehemu ambazo benki haziwezi kuweka matawi kulingana na uwekezaji unaohitajika.
Merchant Point of Sales (POS) Machines, ambazo zinatumia VISA na MasterCard ni mahususi kwa malipo kwenye maduka makubwa (SuperMarkets) Mahoteli na migahawa na pia maduka ya kawaida. Machine hizi hutumika kufanya malipo moja kwa moja toka kwenye akaunti ya mteja badala ya kutembea na pesa taslimu. Merchant Point of Sales (POS) Machines zinapunguza kwa kiasi kikubwa gharama na madhara ya kutembea na pesa taslimu.
DTB-Tanzania kwa sasa ina matawi 28 nchini, 14 kati ya hayo yakiwa jijini Dar es Salaam kama ifuatavyo (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, Nyerere, Kariakoo, Tawi la Nelson Mandela, Upanga lililo barabara ya Umoja wa Mataifa na Tawi la CBD lililo kwenye makutano ya barabara za Samora na Mirambo) jingine ni Tawi Mbezi Chini lililo Kata ya Kawe na tawi jipya kabisa la Mlimani City. Matawi mengine yakiwemo matawi mawili kwa miji ya Mwanza na Arusha na tawi moja katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora, Tanga na visiwa vya Zanzibar.
DTB-Tanzania ni kampuni tanzu ya makampuni ya DTB (DTB Group) yanayoendesha shughuli za kibiashara katika ukanda wa Africa Mashariki nchini Kenya, Uganda na Burundi. DTB Tanzania pia ni kampuni tanzu ya Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi (The Aga Khan Fund for Economic Development – AKFED) ambayo ni tawi la Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network -AKDN)
No comments:
Post a Comment