Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 16 November 2018

WABUNGE WASHAURIWA KUNUNUA HISA ZA BENKI YA DCB


Benki ya Biashara ya DCB ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Godfrey Ndalahwa, watembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma ikiwa ni muendelezo kampeni ya kuhamasisha uuzaji wa hisa zake kwa Wabunge na watanzania wote.

Akizungumza wakati akimtambulisha Mkurugenzi mtendaji huyo pamoja na ujumbe wake, Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai aliwatangazia wabunge hao taarifa za uzinduzi huo na ya kwamba hisa zinaweza kununuliwa katika matawi ya benki hiyo, mawakala wa Solo la Hisa (DSE) kwa bei pungufu ya shs 265 na ya kwamba benki hiyo sasa ni benki ya biashara.

DCB ilizindua zoezi la kuuza hisa zake Novemba 12 mwaka huu huku mwanahisa namba moja Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa akiwa mteja wa kwanza kujitokeza kununua hisa.

No comments:

Post a Comment