Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 16 November 2018

CBA BANK NA VODACOM WAFANYA PROMOSHENI YA PILI YA SHINDA NA M-PAWA IKIWA NI MOJA YA JITIHADA ZA KUHIMIZA WATANZANIA KUWEKA AKIBA NA KULIPA KWA WAKATI

Mkurugenzi wa Idara ya Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika (CBA) Julius Konyani (katikati), na muwakilishi kutoka Vodacom Tanzania Noel Mazoya, katika uzinduzi rasmi wa Promosheni iliyopewa jina la Shinda na M-PAWA. ilifatwa na kutangazwa kwa washindi 400 waliongezewa mara mbili ya salio lao, na watu 30 zaidi waliochukua mikopo na kulipa kwa wakati walijishindia 100,000 tshs kila mmoja.
Dar es Salaam, 12 Novemba 2018 - CBA Bank na Vodacom wamefanya promosheni ya pili ya Mpawa iliyoibua washidi wengine 200 walioweka amana na Mpawa, ambao watajishindia mara mbili ya kiasi walichohifadhi kwenye Mpawa.

Promotion hii ilizinduliwa tarehe 8 mwezi wa kumi na moja, Draw ya leo inafanya idadi ya washindi kuwa 430, Ambapo washindi 400 wamejishindia mara mbili ya amana zao walizohifadhi kwenye Mpesa, na washindi 30 ambao walikopa na kurejesha kabla ya wakati wamejishindi Shilingi TZS 100,000/= kila mmoja. Jumla ya washidi 1296 wanategemea kupatikana katika kipindi hiki cha wiki sita za kampeni. Zawadi kubwa zitakazotolewa kwenye droo kubwa wiki ya sita zitakua ni kitita cha Milioni 10 taslimu na Bajaj tano.

Promosheni hii inaonyesha jitihada za CBA Bank na Vodacom kuleta muamko wa kifedha na kuhimiza Watanzania kuwa na tabia ya kuweka akiba. Akizungumza wakati wa uzinduzi kutoa zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CBA Julius Konyani alisema “M-PAWA ni bidhaa inayoendelea kuleta mapinduzi ya kimaendeleo kwa Watanzania hasa wale wamiliki wa biashara ndogo wanaoweka akiba na na kupata riba na Pia kupata mikopo inayowasaidia katika kuendeleza na kukuza biashara zao”.

Promosheni hii ya Shinda na M-PAWA itaendeshwa kwa muda wa wiki sita kuanzia Novemba 2018 hadi nusu ya Desemba 2018.

Meneja Masoko wa Vodacom Huduma za kifedha Noel Mazoya alisema “Wateja watakaoomba mkopo na kurudisha mapema watakuwa na nafasi ya kuopoa zawadi ya shilingi 100,000 kwa wateja 15 kila wiki na Jumla ya wateja 96 watashinda kwa wiki sita. Tunajenga utamaduni wa kuhimiza Watanzania kuchukua mikopo ili kuwawezesha kukuza biashara zao. Hata hivyo hatuwahimizi tu wateja wakope, lakini pia kurudisha mikopo mapema. Hii itawapa wateja fursa ya kuomba tena mkopo na kuongeza kiwango wanachoweza kukopa” alisema haya wakati wa tukio la droo ya kwanza lililoshuhudiwa na Bodi ya bahati nasibu Tanzania pamoja na watendaji wengine wa CBA.

Mpawa ni Huduma inayotolewa kwa ushirikiano wa Bank ya CBA na Vodacom, Huduma hii inawewezesha wateja kuweka fedha kwenye Mpawa na Kupata Riba/faida. CBA imekuwa mmojawapo ya benki inayowekeza nchini ambapo kuptia huduma hii imefanikiwa kuwafikia wateja zaidi ya milioni saba, wakiwa ni wateja wadogowadogo ambao wanahifadhi kiwango cha kati ya shilingi 1000/= na 3000/=. Viwango ambavyo mfumo wa kibenki wa kisasa usingeweza kuwahudumia, Huduma hii ya mpawa imeifikia jamii kubwa ambayo haipo kwenye mfumo rasmi wa kifedha (Financial Inclusions). CBA Bank na Vodacom zitaendelea kuwekeza nchini na wanatoa wito kwa wateja wote wa Vodacom/Mpesa kuweka hela zao katika kibubu chao cha mpawa ambacho ni salama na benki yao mkononi mwao, Pia wanaweza kukopa kiwango chochote kati ya shilingi 1000 mpaka laki tano.

No comments:

Post a Comment