Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert

Ultimate Finance Advert

Advertise Here

Advertise Here

Wednesday, 14 November 2018

BENKI YA BIASHARA YA DCB YAZINDUA UUZAJI WA HISA ZAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa (kulia), akikabidhi hundi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka baada ya kununua hisa za benki hiyo muda mfupi baada ya DCB kuzindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa. Uzinduzi huo unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa (kulia), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka ofisini kwake Dar es Salaam hivi karibuni wakati akinunua hisa za benki hiyo muda mfupi baada ya DCB kuzindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018. Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenbzi wa DCB, Prof. Lucian Msambichaka (wa tano kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa uuzaji hisa za benki hiyo kwa mwaka 2018 jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa na maofisa wengine wa benki hiyo. Uzinduzi huo unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Biashara ya DCB, Zacharia Kapama (kushoto), akizungumza katika hafla ambayo DCB ilizindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
Baadhi ya wafanyakazi wa DCB na waalikwa wengine wakihudhuria halfla hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi DCB, Prof. Lucian Msambichaka (katikati), akipozi kwa picha ya kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na waalikwa wengine baada ya tukio la uzinduzi wa uuzaji wa hisa za benki hiyo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment