Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 29 September 2018

USHIRIKI WA BENKI YA NBC KATIKA MAONYESHO YA MADINI MKOANI GEITA WAWAVUTIA WENGI

Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage (kushoto) akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC, wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita hivi karibuni. NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akipokelewa na Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, NBC, Japhet Mazumira (kulia), wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanaliyofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe (katikati) akisaini kitabu cha wageni katika banda la Benki ya NBC wakati alipotembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert na kushoto ni Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira. NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage (katikati) akishikana mikono na Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira, wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka.

Ofisa Mahusiano ya Wateja wa Benki ya NBC Tanzania, Esther Kahabi akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika Kliniki ya Biashara ya NBC iliyooandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na TanTrade katika maonyesho hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka (kushoto) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini kutoka Mkoa wa Geita wakati wa Kliniki ya Biasharaya NBC iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na TanTrade wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Kushoto kwake ni, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert na Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Geita (GEREMA), Michael Kadeo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini wakati wa Kliniki ya Biashara ya NBC iliyooandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na TanTrade ili kuwapa mbinu wa ujuzi katika biashara zao wakati wa maonyesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita.

No comments:

Post a Comment