Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 27 September 2018

BANCABC YASISITIZA AHADI YA KUENDELEA KUTOA BIDHAA ZA KIPEKEE KWA WATEJA WAKE

Mkurugenzi Mtendaji wa Atlas Mara Group Mr. John Staley akiongea na wateja, wanahisa na wafanyakazi wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam hivi karibuni, kwa lengo la kusisitiza ahadi ya kuendelea kutoa bidhaa za kipekee haswa kwa “retail banking” ambayo anajivunia uzoefu wake. Stejini ni muwakilishi wa wanahisa Mr. Michael Wilkerson na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa BancABC Mr. Imani John.
Muwakilishi wa wanahisa wa BancABC Mr. Michael Wilkerson, akizungumza na wateja pamoja na wadau wa BancABC wakati wa mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena Dar es Salaam. Mkutano huo ulikuwa mahususi kwa ajili ya kusisitiza juu ya ahadi ya BancABC kuendelea kutoa na kutengeneza bidhaa bora kwa ajili ya wateja wake. 
Wateja wa BancABC walipowasili kwa ajili ya hafla. Hafla hii iliwaleta pamoja wanahisa, wateja, uongozi pamoja na wafanyakazi wa benki.
Katika picha ya pamoja, toka kulia Mkurugenzi mtendaji wa Atlas Mara Group Mr John Staley, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Mr. Imani John pamoja na muwakilishi wa wanahisa wa BancABC Mr. Michael Wilkerson.
Wafanyakazi wa BancABC katika picha ya pamoja baada ya hafla yenye mafanikio iliyoandaliwa na BancABC.

No comments:

Post a Comment