Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 30 August 2018

AIRTEL, BENKI YA LETSHEGO NA JUMO WAUNGANA ILI KUWEZESHA WATEJA WAO KUWEKA AKIBA KUPITIA TIMIZA AKIBA

Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa TIMIZA AKIBA ambayo ni huduma itakayowezesha wateja wa Airtel Money kujiwekea Akiba wao wenyewe kwa kutumia simu zao za mkononi wakiwa mahali popote. Huduma ya TIMIZA AKIBA ni ushirikiano baina ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania.
Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon wa kwanza kushoto, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Benki Kuu ya Tanzania James Masoy wa pili kulia, Mkurugenzi wa biashara JUMO Tanzania Townsend Rose wa kwanza kulia na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki Letshego Tanzania Simon Jengo kwa pamoja wakionyesha bango baada ya kuzindua TIMIZA AKIBA ambayo ni huduma itakayowezesha wateja wa Airtel Money kujiwekea Akiba wao wenyewe kwa kutumia simu zao za mkononi wakiwa mahali popote. Huduma ya TIMIZA AKIBA ni ushirikiano baina ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Benki Kuu ya Tanzania James Masoy akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa TIMIZA AKIBA ambayo ni huduma itakayowezesha wateja wa Airtel Money kujiwekea Akiba wao wenyewe kwa kutumia simu zao za mkononi wakiwa mahali popote. Huduma ya TIMIZA AKIBA ni ushirikiano baina ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania.
  • Airtel Money, Benki ya Letshego na Jumo wazindua huduma maalum kwa wateja wao kuweka akiba kupitia Timiza 
  • Akiba. Airtel, Benki ya Letshego na Jumo wawajengea wateja wao utamaduni wa kuweka akiba kupitia Airtel Money
Dar Es Salaam 30 Agosti 2018: Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania wamefanya ushirika wa pamoja na kuzindua huduma kabambe itakayowawezesha wateja wao kuweza kujiwekea akiba wao wenyewe kwa kutumia simu zao za mkononi wakiwa mahali popote. TIMIZA Akiba ni huduma rahisi, isiyo na makato na itakayompa mteja zawadi ya fedha kila mwezi kwa kujiwekea akiba binafsi ili kufikia malengo. Zawadi hii itakuwa ni kiasi cha asilimia 5% ya salio l mteja aliloweka kama akiba ili kuhamasisha ari na ukuaji wa akiba.

Huduma hiyo maalum itakayojulikana kama TIMIZA AKIBA imezinduliwa leo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania wakati wa hafla maalum iliyofanyika katika ofisi za Airtel Makao Makuu. Huduma ya Timiza Akiba itakuwa suluhisho kwa wateja kuweza kuweka akiba kupitia simu zao za mkononi ambapo kwa sasa inapatikana kwa wateja wote wa Airtel Money. Wateja wa Airtel Money wataweza kujiwekea akiba zao bure kabisa kuanzia kiwango cha chini kabisa cha TSH100 na watakuwa wanapata riba kila mwezi. Huduma ya TIMIZA Akiba inatumia mfumo usiotoza ada wala gharama za uendeshaji kwani baada ya mteja kupata gawio la faida yake ya akiba ya kila mwezi mteja ataendelea kubaki na kiasi kilekile alichojiwekezea. Mfumo huu wa uendeshaji wa huduma hii ya Timiza Akiba unadhamiria kukamilisha lengo la ushirikiano kati ya Airtel, Benki ya Letshego na JUMO la kuendelea kutumia teknolojia na kubuni huduma bora zaidi ili kuongeza kasi ya utoaji wa huduma jumuishi za kifedha kwa Watanzania.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutambulisha huduma ya TIMIZA AKIBA, Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Benki Kuu ya BoT James Masoy alisema ni faraja sana benki ya biashara, kampuni ya simu pamoja na kampuni ya mikopo midogo midogo kukaa pamoja na kushirikiana kufikisha huduma za fedha kwa wananchi. ‘Mmeamua kuweka ushindani wa kibiashara pembeni na kujumuika pamoja kuhudumia wananchi katika kuunga mkono Mpango wa Serikali wa Huduma za Kifedha Shirikishi’, alisema Majoy.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso, alisema “Airtel Tuna furaha kwa kuendelea kuwahudumia zaidi wateja wetu kupitia TIMIZA Akiba, tunaamini huduma hii itawawezesha kujiwekea akiba zao kwa uhakika zaidi. Tumedhamiria kuendeleza ubunifu kila siku ili kurahisisha huduma za kifedha hapa nchini ziendelee kuwa rahisi na kuwanufaisha watu wengi pale wanapozitumia. Tunataka huduma zetu ziwe sambamba na mahitaji yao na ziwe suluhisho la mipango ya wateja wetu ya baadae”

“Wateja watakaoamua kutenga na kuweka kiasi kidogo cha fedha zao kama akiba badala ya kutumia fedha zote watapata zawadi. Tukijua Kabisa kwamba leo hii watu wengi hawana utamaduni wa kujiwekea akiba, TIMIZA Akiba inatupa Watanzania fursa ya kujiwekea akiba ambayo itatusaidia kukabiliana na dharura na majanga yasiyotarajiwa kwa siku za baade”. Alielezea Colaso

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Letshego Bank Tanzania, Thabit Ndilahomba, amesema, “Timiza Akiba ni matokeo ya ushirikiano wa kweli unaolenga kuboresha maisha ya wateja kama ilivyo ahadi yetu ambayo ni (Lets Improve Lives). Ushirikiano unabaki kuwa nyenzo yetu muhimu katika nchi zote 11 tunazoendesha shughuli zetu Afrika ikiwemo Tanzania. Tukiwa pamoja na Airtel na JUMO, tunatarajia kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba na kuongeza manufaa ya kuweka akiba kwa Watanzania wote, popote walipo.”

Nae Mkurugenzi wa Huduma wa JUMO Tanzania James Townsend-Rose, amesema, “Malengo yetu kama JUMO ni kuhakikisha tunatoa zaidi huduma mahsusi na madhubuti za fedha kwa watu ambao wakati mwingine ilikuwa ni vigumu kwao kupata huduma rasmi za fedha. Timiza Akiba ni mfano mmoja tu wa kile tulichoweza kufanikiwa kukifikia wakati tunajiandaa kuwapa thamani halisi wateja wetu kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za fedha.”

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Airtel Tanzania
Jackson Mmbando – Meneja Uhusiano na Mawasiliano
jackson.mmbando@airtel.co.tz 
Mobile +255 786670120

Letshego Tanzania
Silvester Mhilu – Meneja Masoko na Mawasiliano n
SilvesterM@letshego.com
Mobile: +255 718611748

Jumo
Name – James Townsend-Rose
Mkurugenzi wa Huduma Jumo

KUHUSU BHARTI AIRTEL LIMITED

Bharti Airtel Limited ni kampuni ya kimataifa inayoongoza kutoa huduma za bora za mawasiliano ya simu za mkonono na inaendesha shughuli zake katika nchi 16 za Asia na Afrika. Makao makuu yake yapo New Delhi, India, kampuni hii ni miongoni mwa watoa huduma bora za mawasiliano duniani na inashika nafasi ya 3 kati ya kampuni zenye idadi ya wateja wengi. Nchini India, huduma za kampuni hii hujumuisha bidhaa za mawasiliano za 2G, 3G na 4G, biashara ya simu, broadband ya nyumbani yenye kasi, DTH, huduma za biashara ikiwa ni pamoja na huduma za kitaifa na kimataifa za umbali mrefu kwa wasafiri. Katika maeneo yote ya kijiografia, inatoa huduma za wireless za 2G, 3G, 4G na biashara ya simu. Bharti Airtel alikuwa na wateja zaidi ya milioni 456 katika shughuli zake mwishoni mwezi Juni 2018. Ili kujua zaidi tafadhali tembelea, www.airtel.com

KUHUSU JUMO

JUMO Tanzania Limited ni sehemu ya kampuni ya JUMO, kampuni inayoendesha shughuli zake katika nchi kadhaa bara Afrika na Asia. JUMO inaendelea kutoa jukwaa la kuunganisha watu kwenye mifumo rasmi ya huduma rahisi na nafuu za fedha duniani. Hili limeiwezesha JUMO na washirika wake kuweza kutoa huduma za mikopo na akiba kwa mamilioni ya watu duniani ambao mwanzo walikuwa hawana fursa ya kupata huduma hizi katika benki za kawaida. Kwa taarifa zaidi tembelea www.jumo.world

KUHUSU LETSHEGO BANK

Letshego bank (T) Ltd. Ni sehemu ya mtandao wa taasisi za fedha unaoitwa Letshego Holding Limited (LHL), yenye leseni ya Benki Kuu ya Tanzania inayoipa kibali cha kuendesha shughuli zake kama benki ya biashara. Letshego Bank inatoa huduma hafuu za fedha na zenye tija katika sekta ya elimu, afya, nyumba na makazi na kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati. Letshego inatoa huduma zake nchini kupitia mtandao wa matawi, huduma za benki kupitia simu, huduma za wakala na kwa njia ya ATM.

KUHUSU LETSHEGO HOLDINGS LIMITED (“LETSHEGO GROUP”)

Letshego Holding Ltd, ni mtandao wa taasisi za fedha iliyoandikishwa kwenye soko la hisa la Botswana, makao makuu yake yapo yenye lengo la kutoa huduma jumuishi za fedha kwa kwa watu wenye kipato cha chini na kati katika nchi 11 inakofanya shughuli zake kusini mwa jangwa la sahara. Ikiwa na jumla ya wafanyakazi wa zaidi ya 3000 na jumla ya wateja zaidi ya laki nne , Letshego inaamini katika matumizi ya teknolojia katika kuwezesha kuwafikia watu wengi zaidi na kufanikisha utoaji wa huduma zinazoboresha maisha kwa watu.

Mwaka huu (2018), Letshego inaadhimisha miaka 20 ya kutoa huduma kwa lengo la kuunga mkono juhudi za maendeleo ya jumuiya mbalimbali za Afrika kwa nia ya kufikia malengo ya kuwa taasisi ya fedha inayoongoza kwa utoaji wa huduma jumuisho za fedha Afrika.

Kwa taarifa zaidi tembelea www.letshego.com

No comments:

Post a Comment