Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 22 February 2018

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO MAALUM WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) UNAOFANYIKA KAMPALA NCHINI UGANDA. FEBRUARI 22, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika Kampala nchini Uganda. Februari 22, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wa nne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipokuwa ukipigwa katika ukumbi wa mkutano uliopo katika eneo la Munyonyo Kampala nchini Uganda. Februari 22, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wanne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati wa mkutano huo Maalumu wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unao endelea jijini Kampala. Februari 22,2018.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni akifungua Mkutano huo maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Kampala nchini Uganda. Februari 22, 2018.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika picha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, pamoja na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir mara baada ya Mkutano Maalum wa 19 wa Jumuiya hiyo uliofanyika Kampala nchini Uganda. Februari 22, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir kabla ya kuanza kwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Februari 22, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja katika eneo la Munyonyo Kampala nchini Uganda. Februari 22, 2018.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment