Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 16 February 2018

FINCA NA MASTERCARD FOUNDATION WAFANYA MKUTANO WA USHIRIKISHAJI WA KIFEDHA JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akifungua kongamano la huduma jumuishi za kifedha wenye lengo la kukuza upatikanaji wa huduma hizo kupitia mifumo ya teknolojia za kidijitali kati ya benki ya FINCA na MasterCard Foundation lililofanyika jijini Dar Es Salaam leo. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) na Naibu Gavana wa Benki Kuu, Yamungu Kayandabila (wapili kushoto) wakiwa na picha walizokabidhiwa kutoka kwa Afisa Mtendaji mkuu wa Benki ya FINCA Tanzania, Issa Ngwegwe (wapili kulia). Wengine wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji FINCA Canada, Stephanie Emond na mwisho kushoto ni Mkurugenzi Uendeshaji wa FSDT, Irene Majede Mlola. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Kongamano la huduma jumuishi za kifedha wenye lengo la kukuza upatikanaji wa huduma hizo leo jijini Dare Es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya FINCA Tanzania, Issa Ngwegwe akizungumza kwenye Kongamano la huduma jumuishi za kifedha wenye lengo la kukuza upatikanaji wa huduma hizo leo jijini Dare Es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji FINCA Canada, Ms.Stephanie Emond akizungumza kwenye kongamano.
Mkurugenzi Uendeshaji wa FSDT, Irene Majede akielezea jambo kwenye kongamano la Huduma Jumuishi za Kifedha leo.
16 February 2017, Dare es Salaam - Benki ya kutoa mikopo midogo midogo inayoongoza Tanzania FINCA Micro-Finance Bank, kwa kushirikiana na MasterCard Foundation, taasisi ya kimataifa ambayo inatoa ushirikishaji wa kifedha na kuendeleza elimu kwa vijana barani Africa, leo imefanya mkutano wa siku moja wa Ushirikishaji wa Kifedha jijini Dar es Salaam wenye lengo la kushirikishana ujuzi miongoni mwa wadau mbalimbali katika kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia katika mifumo mbalimbali ya kidigitali.

Mkutano huo, ulilenga kutathmini mafunzo yaliyotolewa kwa miaka mitano ya ushirika baina ya FINCA na Mastercard Foundation kwa lengo la kukuza huduma za kifedha kwa jamii ya watu walio katika sekta isiyo rasmi katika nchi za Tanzania, Zambia na Malawi kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na watoa huduna za kifedha, wafadhili, watafiti na wasimamizi wa sekta za kifedha, kubadilishana mawazo kwa lengo la kukuza upatikanaji na matumizi za huduma za kifedha Tanzania.

Katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo,  Afisa Mtendaji Mkuu wa FINCA, Tanzania, Issa Ngwegwe alisema “mifumo ya teknolojia ya kidigitali ni kichocheo kikubwa sana katika ushirikishaji wa kifedha na pia maendeleo ya mfumo wa kidigitali ni muhimu katika kuongeza upatikanaji wa huduma hizo.”

"Mifumo ya kidigitali ya simu za mkononi na wakala wa kibenki ni vipengele muhimu katika kupunguza bei ya kuwafikia mamilioni ya watanzania ambao hawana huduma za kibenki. Ushiriki na mitandao ya simu inaonyesha fursa ya kukuza upatikanaji wa huduma za kifedha. “ Aliongeza.

Akiongea katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendji wa wa FINCA Canada Bi. Stephanie Emond alisema kwamba ushiriki wa Mastercard Foundation umeweka misingi mizuri ya ukuwaji kwa kupitia matumizi ya teknolojia ya kifedha na mafunzo kwa lengo la kuboresha huduma na kukuza uwezo wa FINCA pamoja na uelewa mzuri zaidi wa mahitaji ya wateja na matokeo ya mipango ya ushirikishwaji wa fedha kwa.

“Tunaamini kwamba kupitia mkutano huu tutajifunza kutoka safari yetu na tujenge uhusiano wa karibu miongoni mwetu pamoja na nafasi nzuri ya kukabiliana na changamoto za soko alikadhalika na kuweka mazingira mazuri kwa ukuwaji wa huduma za kifedha na uendeshwaji wa sekta hiyo.” Alisema Bi. Stephanie.

Kwa upande wa mgeni rasmi Dr. Ashatu Kijaji, Naibu waziri wa  fedha na Mipango alisisitiza kuwa serikali imekusudia kukuza ushirikishaji wa kifedha kupitia uwekaji wa kanuni stamilifu na uratibu mzuri pamoja na mazingira mazuri kwaajili ya ushirikishaji wa kifedha ambao utapeleka huduma za kifedha  kwa watu maskini kukiwa na hatua stahiki za kumlinda mtumiaji.    

Kuhusu FINCA
FINCA ni Taasisi ya kimataifa inayolenga kukomesha umasikini kupitia suluhu za kudumu ambazo zinasaidia watu kujipatia ajira, mali na kujikwamua kimaisha. FINCA inaifikia jamii kupitia mtandao wenye zaidi ya taasisi ndogondogo na mabenki 20 zinazotoa huduma ya kibenki kwa zaidi ya wateja milioni mbili katika mabara matano.
Tangu mwaka 2013, FINCA imeshirikiana na taasisi ya Mastercard Foundation kukuza ushikishwaji wa kifedha barani Afrika.
Twitter:@FINCA

Kuhusu MasterCard Foundation
MasterCard Foundation ni taasisi huru ya kimataifa yenye makao yake makuu jijini Toronto, Canada, yenye thamani ya zaidi ya $6 billioni Kupitia ushirikiano na taasisi washirika katika nchi 50, inatengeneza fursa kwa watu wote kujifunza na kuendelea.  Programu za MasterCard zinahamasisha ushirikashaji wa kifedha na uendelezaji wa vijana kielimu, hususani barani Afrika. MasterCard Foundation ilianzishwa mwaka 2006.
www.mastercardfdn.org@Mastercardfdn

No comments:

Post a Comment