Punde tu baada ya kumaliza ofa mahsusi ya kufunga mwaka, MultiChoice Tanzania leo imetangaza neema kwa wateja wake wapya watakaojiunga kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka ambapo watajipatia ofa ya kifurushi kwa muda wa miezi miwili bure!
Ofa hiyo ya fungua mwaka inayofahamika kama ‘The Punguzo‘ inaanza rasmi tarehe 1 Februari 2018 na itaendelea hadi mwisho wa mwezi Machi mwaka huu. Katika kipindi hicho wateja wote wapya wa DStv, wataweza kupata vifaa vyote vya DStv kwa shilingi 79,000 tu na kisha kupata ofa ya kifurushi cha miezi miwili bure!
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo katika ofisi za MultiChoice Tanzania, Meneja Masoko Alpha Mria, amesema kuwa ofa hii ni muendelezo wa msururu wa ofa kabambe zinazotolewa na kampuni ya MultiChoice kwa wateja wake.
Amesema tofauti na ofa ya kufunga mwaka ambapo mteja alikuwa anapatiwa mwezi mmoja tu wa bure, sasa hivi ofa ya kifurushi imeongezwa na hivyo mteja mpya sasa anapata kifurushi cha miezi miwili bure.
"Tunatambua kuwa mwanzo wa mwaka unakuwa na majukumu mengi sana ikiwemo malipo ya karo za shule, ada mbalimbali na kadhalika, hivyo tumeamua kuwapa wateja wetu ofa hii ya miezi miwili bure ili kuwapa uhakika wa kuendelea kufurahia habari, sinema, tamthilia na burudani kedekede zipatikanazo katika king’amuzi chao pendwa cha DStv," alisema Alpha.
Ameongeza kuwa kwa shilingi 79,000 tu, mteja anapata vifaa vyote vya kujiunga na DStv ikiwemo Dish, Dikoda, Rimoti, na zaidi ya yote, anapata kifurushi cha miezi miwili bure. Kifurushi ambacho kitamuwezesha kuona channeli zaidi ya 70 huku akifurahia ligi maarufu kama La Liga, Ligi Kuu ya Uingereza, FA Cup, Europa League, burudani ya Mieleka (WWE), filamu na tamthilia kali za kitanzania kama Sarafu, Kapuni, Mwantumu na nyingine nyingi ndani ya Maisha Magic Bongo (160).
Kipindi hiki cha Valentine, watazamaji watapata fursa pia ya kuangalia tamthilia za kusisimua za mapenzi na mahusioano ndani ya chaneli ya Zee World (166), Telemundo (118), Eva+ (142), Televisa, na filamu kibao kutoka nje.
Amewataka wale wote ambao hawajajiunga na DStv kuchangamkia ofa hii kwani itaendelea kwa kipindi cha miezi miwili tu.
No comments:
Post a Comment