Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 31 October 2017

BENKI YA NMB YAFUNGUA MATAWI MAPYA ARUSHA NA MOSHI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Bank PLC, Bi Ineke Bussemaker baada ya uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Ngaramtoni lililopo katika wilaya ya Arumeru katika Mkoa wa Arusha. Uzinduzi wa tawi hili unafanya NMB kua na matawi zaidi ya 212 nchi nzima. Hii ni katika jitihada za kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Bank PLC, Bi Ineke Bussemaker, akiwashukuru wateja wa NMB waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Ngaramtoni lililopo katika Wilaya ya Arumeru ndani ya Mkoa wa Arusha. Uzinduzi wa tawi hili unafanya NMB kua na matawi zaidi ya 212 nchi nzima hii ni katika jitihada za kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira (kati kati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mbuyuni lililopo katika Manispaa ya Moshi mjini. Hafla hii ya Uzinduzi ilifanyika mwishoni mwa wiki. Wa kwanza kulia ni Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini, Salie Mlayi wakishuhudia uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira akizungumza na Meneja wa tawi la NMB Mbuguni, Rose Manyonyi baada ya kutembelea tawi la NMB na kujionea mwonekano wake mara tu baada ya uzinduzi wa tawi la NMB Mbuyuni. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Bw. Abdulmajid Nsekela pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini, Mhe. Kippi Warioba.


No comments:

Post a Comment