Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 15 September 2017

BENKI YA EXIM YATOA MAGODORO NA VITANDA 50 YENYE THAMANI YA MILIONI 20 KWA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA, ZANZIBAR




13 Septemba 2017, Zanzibar - Benki ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 50 yenye thamani ya TZS 20M / - kwa Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyoko Unguja Zanzibar, kama sehemu ya kampeni yake yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.

Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka huu, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza shilingi milioni 200 katika sekta ya afya Tanzania. Mradi huu unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini.

Hospitali ya Mnazi Mmoja, ni hospitali ya pili kupokea mchango huu, baada ya Hospitali ya Temeke Dar es Salaam mwezi uliopita. Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo na mgeni rasmi alikwa Mhesimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Hazina wa benki ya Exim, Bwana Arafat Haji alisema, “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.”

Hospitali na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Takwimu za Shirika la afya duniani ‘WHO’ zinaonyesha kuwa Tanzania ina uwiano wa vitanda saba kwa kila watu elfu kumi. Hivi sasa hali ya kuona wakinamama wajawazito wawili wakitumia kitanda kimoja au wengine kulala sakafuni ni jambo la kawaida katika hospitali hizi.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali wa hospitali ya Mnazi Mmoja, Dkt. Ali Salim alisema, “Pungufu wa vitanda katika hospitali ya Mnazi Mmoja ni changamoto kubwa. Tunahitaji vitanda 100, haswa kwenye wodi ya wazazi, wodi ya kansa na wodi ya vichaa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 50 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii katika hospitali yetu.”

Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Mtwara, Pemba na Unguja.

Benki ya Exim ilitambuliwa kama benki bora kwa huduma ya wateja binafsi mwaka huu na taasisi ya The Banker ya Afrika Mashariki na sasa inasheherekea miaka 20 ya mafanikio, ukuaji na kuwa kiongozi katika kuingia katika masoko mapya barani Afrika. Benki ya Exim ilianzishwa mwaka 1997 na imetanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu katika nchi za Comorro (2007), Djibouti (2010) na Uganda (2016). Benki hii inajivunia kuwa ya kwanza ya Kitanzania kuingia katika masoko ya nje ya nchi. Lengo muhimu kwa benki hiyo ni kutengeneza thamani ya uwekezaji kwa wanahisa wake na kufanikisha ukuaji kupitia utoaji wa huduma za tofauti na zinazomfaa mteja.

Mwaka jana benki ya Exim ilipata faida kabla ya kodi ya kiasi cha shilingi 83.3 bilioni ikiiweka benki hiyo kwenye nafasi ya nne kwa mtaji nchini Tanzania. Katika kipindi cha miaka 19 ya kuwepo sokoni benki hiyo imejenga taasisi imara kijiografia, katika bidhaa za kivumbuzi, mahusiano mazuri na wateja na uwezo wake wa kutoa huduma kwa haraka zaidi.

No comments:

Post a Comment