Kamanda wa Polisi wa kikosi cha
Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akizungumza na
wafanyakazi wa Zantel walipomtembelea katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini
Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi
mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani.
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha
Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP Theopista Mallya akiwaonyesha
wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel picha iliyotumwa na wadau wa
usalama barabarani inayoonyesha matumizi mabaya ya barabara yanayofanywa na madereva
wazembe. Wafanyakazi hao walifanya ziara katika kituo cha Polisi cha Oysterbay
jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhitimisha matembezi
mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Kushoto
ni Mkuu wa Sheria na Manunuzi Zantel, Rehema Khalid.
Askari wa Usalama barabarani, Wilaya
ya Kinondoni S/SGT Rehema (kulia) akieleza kuhusu masuala ya usalama barabarani
kwa wafanyakazi wa Zantel katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es
salaam mwishoni mwa wiki mara baada ya wafanyakazi hao kukamilisha matembezi mafupi
ya kuadhimisha siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Waliokaa Kushoto
ni Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni
ACP Theopista Mallya na Afisa Mkuu wa masuala ya kiufundi Zantel, Larry Arthur.
Mkuu wa Kitengo cha Intaneti na Simu
wa Kampuni ya Mawasiliano Zantel, Hamza Zuheri (Kushoto) akifafanua jambo kwa
Kamanda wa Polisi wa kikosi cha Usalama barabarani wa Wilaya ya Kinondoni, ACP
Theopista Mallya (Wa pili kulia) ambapo wafanyakazi wa Kampuni hiyo walimtembelea
Kamanda huyo katika kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishoni
mwa juma mara baada ya kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya Afya
na Usalama mahali pa kazi duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Mawasiliano ya Zantel, Benoit Janin akizungumza na wafanyakazi wake mara
baada ya wafanyakazi hao kuhitimisha matembezi mafupi ya kuadhimisha siku ya
Afya na Usalama mahali pa kazi duniani. Hafla hiyo ilifanyika katika makao
makuu ya Kampuni hiyo Msasani jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
No comments:
Post a Comment