Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (wa tatu kushoto)
akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa kampuni hiyo na
wateja kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016
iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo
Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imesema itaendelea
na utekelezaji wa kuboresha miundombinu ya mtandao wake wa simu za mezani,
mkononi pamoja na huduma za data ili kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja
wake na kufikia kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano
nchini.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alipokuwa akizungumza na wateja mbalimbali kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Kaimu
Afisa huyo wa TTCL, alisema kuwa maboresho ya miundombinu yanayofanywa kwa sasa
katika shirika hilo yanaliwezesha kukabiliana na changamoto zilizokuwepo awali
na kuwapa wateja weke fursa ya kufurahia huduma mpya na za zamani zinazotolewa
kisasa na kwa umahiri mkubwa hivi sasa.
"Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inaendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wa simu za mezani, simu za mkononi na huduma za Data ili tuweze kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu na kufikia kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano," alisema Waziri Kindamba.

Aidha alifafanua kuwa TTCL inawaahidi wateja wake na taifa kwa ujumla kwamba itaendelea kutoa huduma bora, za uhakika na gharama nafuu katika kutengeneza mazingira mazuri ya kiteknolojia, kwani baada ya mabadiliko watumishi wake wameazimia kuongeza kasi ya kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu na uzalendo wa hali ya juu ili kwenda sambamba na mahitaji ya sasa na baadaye ya wateja wa sekta ya Mawasiliano.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi
mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa
huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la
kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya
Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu
Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba akizungumza na wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya kilele
cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la
Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias
Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment