Tuzo za makampuni 100 ya kiwango cha kati nchini kutolewa leo katika hafla itakayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City. Hayo
yamebainishwa siku ya jana katika mkutano uliowakutanisha wadau wote
walioshiriki katika mchakato huo pamoja na waandaaji na wadhamini uliofanyika
katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Mchakato huu unaratibiwa
na KPMG na Mwananchi Communications Ltd na kudhaminiwa na Benki M.
|
Mkurugenzi Mkuu wa KPMG Bw. David Gachewa akizungumza katika mkutano huo, KPMG na Mwananchi Communications Ltd ndio waratibu wa mchakato huo chini ya udhamini wa Benki M. |
|
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la biashara la Africa Mashariki (EABC) Bw. Felix Mosha akizungumza na wadau wa tuzo za makampuni 100 ya kiwango cha kati nchini katika mkutano wa wadau uliofanyika jana katika hoteli ya Hyatt Regency. Hafla ya ugawaji tuzo hizo zinafanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City. |
|
Waandaaji wa mchakato wa tuzo za makampuni 100 ya kiwango cha kati nchini wakifuatilia mkutano wa wadau wa tuzo hizo siku ya jana katika hoteli ya Hyatt Regency, kutoka kushoto ni Mhariri Mkuu wa Mwananchi Communications Ltd Bakari Machumu, Mkurugenzi Mkuu wa Research Solutions Africa Jasper Grosskurth, Mkurugenzi wa KPMG David Gachewa na Naibu Mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso. |
No comments:
Post a Comment