Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 16 August 2016

WATEJA WA TIGO PESA KUPATA 5.6BN/- GAWIO LA TISA LA ROBO MWAKA

Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo, Raun Swanepoel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampuni hiyo kugawa faida kwa watumiaji wake wa huduma kwa njia ya simu ambapo ni kiasi cha bilioni 5.6 kwa watumiaji wa Tigo pesa. Kushoto kwake ni Meneja Chapa, William Mpinga katika mkutano uliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita.
Dar es Salaam, Agosti 09, 2016 - Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali, Tigo imetangaza tena gawio la robo mwaka la shilingi bilioni 5.6 kwa watumiaji wa Tigo Pesa ikiwa ni mara ya tisa kwa kampuni hiyo ya simu kugawa faida hiyo kwa watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa njia ya simu.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Huduma za Fedha kwa njia ya simu wa Tigo, Raun Swanepoel alisema kwa ujumla kampuni hiyo imeshalipa watumiaji wake wa huduma za fedha kwa njia ya simu jumla ya shilingi bilioni 46.2 ikiwa ni malipo ya robo mwaka tangu kuzinduliwa kwa huduma hiyo Julai 2014.

Swanepoel alisema kwamba katika robo ya pili ya mwaka huu kiwango cha faida kilipanda na kufikia asilimia 8 kulikosababishwa na kuongezeka kwa kiwango cha hisa katika mabenki mbalimbali ya biashara.

“Faida hii ya hisa inalipwa wateja binafsi, mawakala wa reja reja na washirika wengine wa kibiashara wa Tigo ambao kila mmoja anapokea malipo yake kulingana na thamani ya fedha zilizowekwa kielektroniki ndani ya pochi zao za Tigo Pesa,” alisema Swanepoel.

Swanepoel aliongeza: “Kusema kweli tunafurahi kutangaza ongezeko hili la faida katika gawio la mara ya tisa mfululizo. Hii inaonesha jinsi tulivyojikita katika kuwawezesha wateja wetu kufikia huduma za kifedha pamoja na nchi zima kwa ujumla kupitia huduma za Tigo Pesa”.

Alibainisha ongezeko la faida la Tigo, kuboreshwa kwa mazingira ya soko na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa Tigo Pesa kama moja ya kichocheo kilichosababisha kuongezeka kwa faida hususani kwa upande wa wafanyabiashara. Tigo Pesa hivi sasa ina mtandao mkubwa wa wafanyabiashara zaidi ya 50,000.

Swanepoel alisema kuwa kama ilivyokuwa hapo awali gawio kwa wateja linakokotolewa kwa kuangalia wastani wa salio la kila siku la mteja la Tigo Pesa katika pochi yake ya simu na kuongeza kuwa mpango huu wa kugawa faida umeainishwa katika kanuni za Benki Kuu iliyotolewa February 2014.

Mwaka 2014 Tigo Tanzania ilikuwa kampuni ya kwanza ya simu duniani kugawa faida iliyozalishwa na fedha za simu zilizopo katika Akaunti ya Udhamini kwa kipindi cha robo mwaka kwa wateja wake.





Mwisho

No comments:

Post a Comment