Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez |
Ushindani huu ambao umechochewa na kuingia kwa kampuni mpya katika sekta ya mawasiliano Tanzania, umefikisha jumla kuu ya watumiaji wa huduma ya mawasiliano nchini kufikia 39.8 milioni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Mamlaka ya Mawasilano Tanzania, (TCRA).
Kampuni ya MIC Tanzania Ltd- ijulikanayo kwa jina lingine kama Tigo – ilisajili juma ya wateja wapya 488,886 katika kipindi hicho cha miezi mitatu sawa na asilimia 34.
Idadi hii ya wateja wapya inaifanya Tigo kuwa na jumla ya wateja 11,115,991 na kuifanya kampuni hiyo kuwa katika nafasi ya pili kwa ukubwa imiliki asilimia 28 la soko la mawasiliano nchini na hivyo kuipita Airtel ambayo imekuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha takriban muongo mmoja.
Airtel kwa upande mwingine ilisajili jumla ya wateja wapya wapatao 32,839 katika kipindi hicho cha miezi mitatu na kufikisha jumla ya wateja wake kuwa 11,047,505 ambayo ni sawa na asilimia 28 lakini kiwa imezidiwa na Tigo kwa idadi ya wateja 68,486.
Licha ya kuendelea kupungua kwa idadi ya wateja wake mwaka hadi mwaka, kwa mujibu wa takwimu za TCRA, Vodacom bado inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wateja wapatao 12,714,297 sawa na asilimia 32 ya jumla ya watumiaji wote wa huduma za mawasiliano Tanzania. Idadi ya wateja wa Vodacom imeonekana kushuka kutoka asilimia 45 mwaka 2007 hadi asilimia 41 mwaka 2008 na kufikia asilimia 39 Desemba 2009.
Wadadisi wa sekta ya mawasiliano wanaelezea hali hii kushuka kwa idadi ya wateja wapya miongoni mwa kampuni hizi kuwa kunachangiwa na mabadiliko ya kimikakati ambapo msizitizo mkubwa miongoni mwa kampuni ni kuwalenga Zaidi wateja watumiaji wa huduma za Intaneti kupitia simu zao kama nyenzo kuu ya kukuza mapato tofauti na matumizi ya kuongea na kutuma sms kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, kwa upande wake ameelezea kukua haraka kwa kampuni hiyo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kusema kumechangiwa na sababu mbalimbali zikiwemo ubunifu mkubwa ambao unafanywa katika kendesha kampuni kibiashara.
“Mafanikio ya Tigo yameletwa na sababu nyingi kama vile kuwapa wateja wetu huduma bora na kwa bei nafuu, upatikanaji wa mtandao wetu nchi nzima, utumiaji wa teknolojia ya kisasa, ubunifu na kuwa karibu na wateja,” Gutierrez anasema.
Akifafanua Zaidi kuhusu ubunifu huo, Gutierrez ametaja baaadhi ya huduma na bidhaa zilioanzishwa na kampuni hivi karibuni kama vile kuwapa wateja uwezo wa kufanya miamala ya kibenki kupitia simu zao za mikononi, uwezo wa kutuma na kupokea fedha kutoka mitandao mingine ya mawasiliano, kutuma na kupokea fedha kimataifa na mgao wa faida utolewao kwa watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa kila baada ya miezi mitatu.
Aidha meneja huyo mkuu ametaja vichocheo vingine vya kukua hara kwa Tigo kuwa ni “kubuni huduma zinazolenga kuwapa wateja wetu fursa ya kuishi maisha ya kidijitali zikiwemo huduma kama vile upatikanaji wa Facebook kwa lugha ya Kiswahili, simu zenye menu ya Kiswahili, WhatsApp ya bure na zinginezo,” amesema.
Kampuni ya Tigo kwa mujibu wa Gutierrez inawekeza kiasi cha dola za kimarekani $ 120 milioni kwa mwaka katika kuboresha mtandao wake na kupanua upatikanaji wa huduma zake nchini.
Ametoa mfano wa huduma ya 4G LTE ya Tigo ambayo kwa sasa inapatikana katika miji sita – Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi na Mwanza – na kuelezea kuwepo kwa mkakati wa kufikisha huduma hii katika mji mikubwa yote nchini ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Kwa upande wake kampuni ya Zantel ambayo ni kampuni dada ya Tigo, zote kiwa zinamilikiwa na Millicom, ilirekodi wateja wapya 320,483 katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ta mwaka 2015 na kufikisha jumla ya wateja 1,839,391. Nayo kampuni mpya ya Haloteli ndiyo iliyoongoza kwa kuvuna wateja wengi kipindi hicho wapatao 793,383 na hivyo kufikisha jumla kuu ya waetja wake kuwa 1,226,678 hadi kufikia mwisho wa Desemba 2015.
Ikiwa na wateja milioni 1.56 hadi kufikia mwishoni mwa Desemba 2015, Smart ilikuwa na asilimia nne (4) la soko la mawasiliano ya simu nchini sawa na Zantel wakati kampuni inayomilikiwa na serikali (TTCL) ikiwa inashikilia asilimia moja (1) ya soko hilo.
No comments:
Post a Comment