Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 23 July 2015

KONGAMANO LA PILI LA DIASPORA KUFANYIKA HAPA NCHINI MWEZI AGOSTI, 2015

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Rosemary Jairo akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa Habari juu ya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora and SMEs partnership 2015) litakalofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015, likiwa na kaulimbiu isemayo 'Creating Linkages between Diaspora and local SMEs in Tanzania'.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea. (Picha na Reginald Philip)
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade Centre UN-Agency) inafanya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora & SMEs Partnership Conference 2015). Kongamano husika litafanyika hapa Dar es Salaam, kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015 katika Hoteli ya Serena. Kongamano hilo litakuwa la pili kufanyika hapa nchini na litahusisha Diaspora na Wadau wa hapa Tanzania.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ndio Wadau Wakuu katika Maandalizi ya Kongamano hili.


Kongamano la mwaka huu lina Kauli Mbiu, ‘Creating Linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania’na Dhumuni lake ni kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara Ndogo na za Kati hapa nchini. Kongamano la mwaka huu pia litahusisha Mikoa ya Tanzania ambapo Mikoa itapata fursa ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mikoani.

Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Aidha, katika kuhitimisha kilele cha Kongamano hilo, Diaspora wanatarajiwa kufanya ziara Zanzibar tarehe 15 Agosti 2015, ikiwa ni sehemu ya mwaliko maalum kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pamoja na Shughuli za Ufunguzi na Kilele, Matukio muhimu yatakuwa ni Maonesho ya Kibiashara, Majadiliano ya Mada kuhusu Ushirikishwaji wa Diaspora kwa Maendeleo ya Nchi hususan SMEs, uwekezaji Mikoani n.k.

Kongamano hilo litahudhuriwa na Watanzania Wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) na wale waliorejea hapa nchini na Wadau wa Maendeleo kutoka hapa nchini.

Wizara ya Mambo ya Nje inawakaribisha kushiriki nasi katika Kongamano hilo. Tafadhali tembeleeni tovuti ya (www.tzdiaspora.com) kupata taarifa muhimu hususan kuhusu Ada za Ushiriki, fursa za Kufadhili na namna ya kujisajili.

Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, 
Dar es Salaam
21 Julai, 2015

No comments:

Post a Comment