Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday 31 May 2015

WAZIRI MEMBE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akifungua rasmi Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Mei, 2015. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC utakaofanyika tarehe 31 Mei, 2015, pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa zitakazowasilishwa na Jopo la Watu Maalum wanaofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi, Taarifa ya Wanasheria Wakuu kutoka Nchi Wanachama na Taarifa ya Mawaziri waliotembelea nchini Burundi hivi karibuni kwa ajili ya kutathmini hali. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera.
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb.) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri.
Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (katikati) ambaye anaongoza ujumbe wa Serikali ya Burundi kwenye mkutano huo wa Baraza la Mawaziri.
Ujumbe wa Uganda ukifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Membe (hayupo pichani).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed (wa pili kushoto) akiongoza ujumbe wa Kenya wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa EAC.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (wa pili kulia mstari wa kwanza) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent Shiyo (kushoto) nao wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri iliyotolewa na Waziri Membe (hayupo pichani).

No comments:

Post a Comment