Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 2 March 2015

HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA YAPOKEA USHURU WA ASILIMIA 0.3 KUTOKA MGODI WA BUZWAGI

Kaimu Meneja Mkuu wa mgodi wa Buzwagi ulio chini ya Kampuni ya ACACIA, Ing. Mutereko Muganda (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania millioni 800 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Bw. Felix Kimaryo (kulia) nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mh. Benson Mpesya (wenye tai).
Kampuni ya ACACIA kupitia mgodi wake wa Buzwagi uliopo kwenye halmashauri ya mji wa Kahama, imeipatia ushuru wa asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi halmashauri hiyo, ikiwa ni ushuru kwa kipindi cha miezi sita (Julai - Disemba, 2014) ambayo ni zaidi ya shilingi za kitanzania millioni 800, uliokabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama.

No comments:

Post a Comment