Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 20 March 2015

BENKI YA NMB YAWAPA MAFUNZO WAJASIRIMALI WILAYA YA ILALA

Benki ya NMB imeendela kuwapiga msasa wateja wake wa mtandao wa NMB Business Club Wilaya ya Ilala kwa kuwapa mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara zao, fedha za kigeni, bidhaa na huduma zitolewazo na benki ili kuwawezesha kuendelea kuwa vinara wa biashara.


Mhazini wa NMB Kanda ya Dar es Salaam kitengo cha Hazina, Joseph Funuguru akitoa mafunzo juu ya fedha za kigeni kwa wateja wa NMB walio katika mtandao wa NMB Business Club katika semina hiyo.
Kaimu mwenyekiti wa NMB Business Club Wilaya la Ilala, Dar es Salaam Bw. Chatele Eliakimu Sando akielezea jinsi wana NMB Business Club Wilaya ya Ilala walivyonufaika na klabu hiyo tangu kuanzishwa kwake na wanavyoendelea kufurahia huduma na bidhaa kutoka benki ya NMB. Akitoa shukurani kwa niaba ya wanachama wake kwa uongozi wa benki ya NMB kwa kuandaa semina ambazo zinatoa mafunzo yanayowajenga wanachama wa NMB Business Club.

No comments:

Post a Comment